Watumishi watatu wa tbs washikiliwa kwa kosa la kumtapeli mmiliki wa kiwanda

    

Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Katikati) akizungumza
leo na wandishi wa habari makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania
(TBS) Jijini Dar es Salaam.




Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Katikati) akizungumza leo na
wandishi wa habari makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Jijini Dar es Salaam.

 

 NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe, ameiagiza Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa shirika
hilo kupisha uchunguzi baada ya kujihusisha na utapeli katika kiwanda
cha Smart industries Limited kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza
na wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mhe.Kigahe ameitaka TBS
kuchukua hatua za kinidhamu kwa watuhumiwa hao kulingana na taratibu na
sheria za mtumishi wakati kesi hiyo inaendeshwa na TAKUKURU pamoja na
jeshi la polisi.


“Mtumishi
mmoja wa TBS ambaye anaitwa Suleimani Banza alienda katika kiwanda cha
Smart industries Limited kilichopo maeneo ya Kijitonyama akiwa na lengo
la kukagua bidhaa ambazo zimepitwa na muda lakini kutokana na kazi zake
yeye si mkaguzi bali ni mtu wa kuweka viwango hivyo aliingilia jukumu
sio la kwake”. Amesema Mhe.Kigahe.


Aidha
Mhe.Kigahe amesema kuwa inasemekana mtuhumiwa huyo aliambatana na watu
walioaminika ni maafisa polisi wakiongozwa na yeye wakiwa na gari la
shirika la TBS kuingia kwenye ukaguzi huo ambao viongozi wa shirika
walikuwa hawana taarifa nao.


“Watu
hao walivyoingia katika kiwanda hicho waliweza kumtishia mwenye kiwanda
kwamba anazalisha bidhaa kwa kutumia malighafi zizilizopitwa na wakati
kwahiyo ili waweze kutokumfungia kiwanda chake anatakiwa awape fedha
Milioni 100”. Amesema Mhe Kigahe.


Pamoja
na hayo Mhe.Kigahe amesema Wizara ya Viwanda iliwachukua watuhumiwa
watatu na kuweza kuwahoji ambao ni Afisa Viwango Suleiman Banza, Dereva
ambaye alitumika kwenda katika kiwanda hicho Issa Mbaruku Dodo, Afisa
Usafirishaji Thomas Elisha Mwankinga ambaye anatuhumiwa kutoa hilo gari
kwenda kutumika katika tuhuma hizo.

Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Katikati) akizungumza leo na
wandishi wa habari makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Jijini Dar es Salaam.