Wawili wafariki dunia mmoja akipigwa jiwe na mwingine kushambuliwa kwa tuhuma za wizi wa mahindi shinyanga

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Watu wawili wamefariki
Dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea Mkoani Shinyanga hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu wakati akizungumza na Misalaba Blog amewataja
watu hao kuwa ni TUMAINI MALIMA mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa
Kambarage Manispaa ya Shinyanga na mwanaume mwingine anayekadiliwa kuwa na umri
wa miaka 35 mpaka 40 ambaye hakufahamika jina na makazi yake.

Amesema TUMAINI MALIMA
amefariki Dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga Mwawaza baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa jiwe na Yohana Daniel akiwa Bar
ya Heinken mjini Shinyanga.

Kaimu Kamanda Nyandahu
amethibitisha kifo cha mtu wa pili   anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 – 40 ambaye
hakufahamika jina wala makazi yake  ameuawa
kwa kushambuliwa na wananchi kwa tuhuma za kuiba Mahindi mabichi shambani
katika kijiji cha Mwamalili kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la
polisi Mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia
ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la polisi
pindi matukio ya uhalifu yanapotokea.