Waziri biteko aipatia kampuni ya madini maagizo mazito

Bei ya rubi - JamiiForums
Madini aina ya Rubi 
WIZARA ya Madini, imetoa muda wa mwezi mmoja kwa kampuni ya uchimbaji madini ya Ruby Mines inayochimba madini ya Ruby ,kijiji cha Mndarara wilayani Longido ,kulipa shilingi milioni 300 inayodaiwa kwa muda wa miaka minane.
Waziri wa Madini, Dotto Biteko, ametoa agizo hilo jana may 15 kwenye eneo la machimbo ya madini hayo katika kijiji cha Mndarara,na kusema kuwa mchimbaji huyo anadaiwa shilingi milioni 300 ambazo zinatokana na malimbikizo ya malipo ya mrahaba.
Waziri ,amemuagiza mchimbaji huyo kuhakikisha analipa deni hilo vinginevyo anyang’anywe Leseni ya uchimbaji madini .
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo, amesema kuwa tangia kuanzishwa kwa soko la madini, mapato yanayotokana na uanzishwaji wa soko hilo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 12 hadi kufikia shilingi bilioni 42.
Amesema kuwa pato hilo limeongezeka kutokana na udhibiti wa utoroshaji madini uliokuwa ukifanywa kwa njia za panya ambapo wafanyabiashara wasiokuwa waadilifu walikuwa wakiyatorosha.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Kampuni ya madini ya Ruby, Devis Shayo,ameiomba wizara impatie muda wa miezi mitatu ili aweze kulipa deni hilo ambalo linatokana na malimbikizo ya mrahaba.
Amesema hivi sasa biashara ya madini imedorora kutokana na ugonjwa wa Corona,na mtiririko wa biashara hiyo umeathirika.