Waziri jaffo apongeza mchakato wa uchaguzi singida

 Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Suleimani Jaffo akizungumza na viongozi wa  Mkoa wa Singida jana, kuhusu
mchakato mzima wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa
utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt. Rehema Nchimbi na Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt. Angelina Lutambi.
 Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Waziri Jaffo.
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP)  Sweetbert  Njewike akiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano na Waziri Jaffo na viongozi wa mkoa huo ukiendelea .
 
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
 
WAZIRI
wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Suleimani Jaffo amewapongeza wakazi wa Mkoa wa Singida kwa kuwa miongoni
mwa mikoa mitano nchini iliyoonyesha hamasa na kujitokeza kwa wingi
kitakwimu katika suala zima la kujiandikishakwenye daftari la kudumu la
mpiga kura, ikiwa ni moja ya hatua muhimu ya mchakato wa uchaguzi wa
Serikali za mitaa unaoendelea.
 
 
Jaffo
aliyasema hayo jana mkoani hapa,alipotembelea kukagua utekelezaji wa
kanuni na taratibu za mchakato wa uchaguzi huo unavyoendelea hatua kwa
hatua.
 
“Katika
mchakato huu wa uandikishaji Singida ni miongoni mwa mikoa mitano
iliyofanya vizuri sana, na kwa wagombea tayari kwa mfululizo wa siku
saba tumekamilisha kuchukua na kurudisha fomu na hatimaye kufanya teuzi
kwa wenyeviti na wajumbe wa kamati za rufaa,” alisema
 
Alisema,
halihalisi iliyopo mpaka jana ni kwamba jumla ya kata 3956 zilizopo
nchi nzima, kimantiki mchakato huo umekwenda vizuri,ingawa kuna baadhi
ya maeneo machache zimejitokeza changamoto ikiwemo baadhiya maeneo
wagombea hawakupata fomu kwa wakati.
 
Aliyataja
baadhiya maeneo hayo kuwa ni Songwe (Vwawa), Arusha (Arumeru), Mwanza
na Kilimanjaro (Moshi), huku akizitaka kamati zote za rufaa nchi nzima
kuhakikisha wakati wa maamuzi wanasimamia haki na usawa, kwa mujibu
kanuni, taratibu na miongozo iliyopo bila ya kumuonea mtu yeyote
 
“Azma
yetu sote ni kuona uchaguzi huu unakwenda na unakamilika vizuri kwa
lengo mahususi la kuunda mamlaka za serikali za mitaa ambazo zina kwenda
kujibu changamoto kubwa za wananchi,” alisema
 
Jaffo
alibainisha umuhimu wa mchakato unaoendelea kwa sasa kuwa,uchaguzi huo
unakwenda kutengeneza serikali za mitaa zilizo karibu zaidi na wananchi,
ambazo taifa likitokana ajenda zozote zile za maendeleo basi
utekelezaji na msingi wa maendeleo utatoka chini.
 
Alisema,
ifahamike kwa wananchi wote kuwa, kwa mujibu wa kanuni
zilizopo,‘Kamatiya Rufaa ya Wilaya’ inaundwa na Katibu Tawala wa Wilaya
(DAS) ambaye ndiye mwenyekiti, akisaidiwa na wajumbe ambao ni watumishi
wanne wa sekta za umma kutoka wilaya zote ndani ya mkoa, huku Katibu  wa
kamati naye atatoka ndani ya sekta ya umma lakini yeye tofauti na
wenzake, ataruhusiwa kupiga kura.
 
“Mwenyekiti
nendeni mkazingatie haki, sikilizeni rufaa na malalamiko yote yatakayo
letwa mezani kutoka vyama vyote, na watu wote kwa uhuru na upana wake
bila kuingiliwa na mtuyoyote,” alisisitiza Jaffo mbele ya wajumbe wa
kamati ya rufaa mkoani hapa, nakuongeza;
 
“mmepewa
rungu lisilo kuwa na mashaka…tendeni haki msiogope akikisheni kila kitu
kinanyooka, kama kuna mtu anastahili haki mpeni na kama kunakasoro
zozote rekebisheni.” 
Zaidi,
alilitaka Jeshi la polisi kupitia Makamanda wa mikoa kuendelea
kusimamia utaratibu uliowekwa kwa misingi ya amani, na kamwe mtu yeyote
asijitokeze kuchafua mchakato wa uchaguzi unaoendelea kwa maslahi yake
binafsi.
 
Mwenyekiti
wa Kamati ya Rufaa mkoani hapa, Wilson Shimo,alisema kwamba wamejipanga
vizuri kusikiliza malalamiko na rufaa zote kwa haki na kurekebisha kwa
mujibu wa kanuni zinazo waongoza, huku akiweka wazi kuwa mpaka jana bado
walikuwa hawaja pokea malalamiko yoyote.
 
Mjumbe
mwingine wa kamati hiyo, Patrick Zamba,alisema watajitahidi kutoa
maamuzi sahihi kwa muda mwafaka kwa mujibu wa sheria na kanuni,
kulingana na kutoridhishwa kwao na maamuzi ambayo yamefanyika.
 
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, alisema siku zote ‘siku njema
daima huonekana asubuhi’ na kwamba hatua ya mkoa huo kupokea hati ya
ushindi na kuwa miongoni mwa mikoa mitano bora ni ishara njema.
 
“Singida
ni njema…tena ni njema….na ni njema sana!… asubuhi hii njema ndio
itabeba mchana wote kuwa mwema zaidi, kwa hatua zote mpaka kukamilika
kwa mchakato mzima wa uchaguzi huu muhimu,” alisema