Waziri mhagama aridhishwa na hatua za ujenzi wa jengo la nec dodoma

NA.MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya
Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedenwa Jijini Dodoma na kusema
ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.

Alikagua
mradi huo, Januari 07, 2020 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Novemba 18, 2019 alipotembelea
na kukagua mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kutoa maagizo
hayo baada ya TBA kusimamisha zoezi la ujenzi kwa ongezeko la gharama
za  kutoka bilioni 13 hadi bilioni  32 na hivyo kumtaka Waziri Mhagama
kufuatilia.

Ziara
ya Waziri Mhagama imebaini maendeleo mazuri ya ujenzi na kufikia hatua
ya asilimia 75 baada ya Tume hiyo kuingia mkataba SUMA JKT kuwapongeza
wakandarasi kwa hatua hiyo wanayoendelea nayo.

“Kwa
kipindi chote ambacho SUMA JKT imeendeela na kazi ya ujenzi wa jengo
hili hali inaridhisha na ni vyema kuhakikisha mnaendana na kasi
inayotakiwa kwa kuzingatia gharama zilizokubalika za bilioni
16,”Alisistiza Waziri Mhagama

Alieleza
kuwa ujenzi wa majengo ya Serikali ni moja ya hatua za kuhakikisha
zoezi la kuhamisha watumishi Dodoma linafanikiwa kwa kuendelea kuweka
miundombinu rafiki ya ofisi zao.

“Mpaka
sasa tayari watumishi wapatao 14868 wameshahamia hapa Dodoma hivyo
tutaendelea kuandaa mazingira ikiwemo ujenzi wa ofisi hizo kwa
kuzingatia kazi ya Uratibu huo ipo chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu,”alisema Mhagama

Alifafanua
kuwa, kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuhakikisha watumishi wa
ofisi hiyo wanatoa huduma vizuri kwa kuzingatia mwaka 2020 ni mwaka wa
uchaguzi mkuu ambapo itasadia utendaji wa kazi.

Waziri
Mhagama ameendelea kueleza kuwa   , miongoni mwa majukumu ya Ofisi yake
ni kuhakikisha inaratibu shughuli zote za kuhamisha watumishi wa
Serikali na kuweka mazingira mazuri ya ofisi zao ili kuendelea
kuitumikia nchi kwa weledi na kujiletea maendeleo yao kwa kutoa wa
huduma bora zinazostahili.

Kwa
upande wake mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa majengo hayo Mhandisi
Michael Mussa alieleza kuwa, wataendelea kufanya kazi kwa viwango
vinavyotakiwa ili kuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia gharama
zilizofikiwa kwenye mkataba wa ujenzi huo.

“Tumefarijika
kwa ujio wa Mhe. Waziri na tunaahidi tutajenga kwa kipindi
kilichopangwa kwa kuzingatia gharama zilizopo kwenye mkataba wa ujenzi
huu,”alieleza Mhandisi Michael.