Waziri mhagama aweka jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha utoaji wa huduma za ukimwi ipogolo

NA. MWANDISHI WETU

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama 
ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Ipogolo Manispaa ya
Iringa ikiwa ni sehemu ya mradi wa uboreshaji wa vituo 20 vitakavyotoa
huduma za UKIMWI kwa wasafirishaji wa masafa marefu.


Hafla
hiyo iliyofanyika tarehe 22 Novemba, 2019 katika Kata ya Ruaha Kijiji
cha Ipogolo mkaoni Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya ,Omari
Badweli (Mb) wa Bahi, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard
Maboko, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe, Mkurugenzi wa Manispaa
ya Iringa, Hamad Ahamad Njovu na wawakilishi kutoka , Ofisi ya Rais
-TAMISEMI , Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,TANROADS pamoja na
watendaji kutoka Halmashauri.

Kabla
ya kuweka Jiwe la Msingi, Waziri Mhagama alipongeza juhudi za Tume ya
Taifa ya Kudhibiti Ukimwi za uratibu na utekelezaji wa masuala ya
mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuhakikisha ujenzi wa vituo 20 unaanza
katika maeneo yenye vichocheo vya maambukizi ikiwemo barabara
zinazotumiwa na wasafirishaji wa masafa marefu.

“Uboreshaji
wa majengo ya Kituo cha Afya cha Ipogolo kwa niaba ya maboresho kama
haya kwenye vituo 20 vilivyoko kando kando ya barabara kuu ya Dar es
Salaam hadi mipaka ya Kasumulu (Tanzania/Malawi) na Tunduma
(Tanzania/Zambia) ili kutoa huduma za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa ufanisi
kwa wasafirishaji wa masafa marefu pamoja na jamii zinazoishi kwenye
maeneo hayo utasaidia kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI kwa
kuzingatia mchango utakaotokana na ujenzi wa vituo hivi”.

Waziri
alieleza, ujenzi huo unaotekelezwa kupitia programu ya sattf barabara
kuu ya Dar es salaam hadi mipaka ya Tunduma/Nakonde (Zambia) na
Kasumulu/Songwe(Malawi) kwa  kutambua umuhimu wa huduma za afya kwa
wananchi wa Tanzania na kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (1977) pamoja na marekebisho yake. Uboreshaji na
utoaji wa huduma bora kwa wananchi ni moja ya utekelezaji wa haki za
binadamu katika kupata huduma za afya na haki ya kuishi.

Aidha
alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi hususani
wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU) wanapata haki ya matibabu ya VVU
na magonjwa nyemelezi, haki ya kutokubaguliwa na haki za kushirikishwa.
WAVIU nao pia wana wajibu wa kulinda wengine wasipate maambukizi ya VVU.

Kwa
kuzingatia Sheria ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (Kuzuia na Kudhibiti)
Na. 28 ya mwaka 2008 na Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 zote
zinatoa wajibu kwa kila mtu kulinda na kutetea haki za WAVIU.

Naye
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwa niaba ya
Mkoa wa mkoa huo Mhe.Ally Hapi alieleza kuwa, ujenzi wa vituo hivyo
utasaidia kupunguza maambukizi na kuongeza tija katika huduma
zitakazotolewa kupitia vituo hivyo.

“Ujenzi
wa kituo hiki uwe chachu ya kuendelea kutumia huduma za Ukimwi ikiwemo
matumizi sahihi ya dawa za kufubaza virusi ili kuendelea kuwa na afya
njema na kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo nchini’”alisema
Kasesela

Kwa
Upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela alieleza kuwa, jamii
haina budi kuendeea kuunga mkono jitihada hizo na kuhakikisha tatizo la
unyanyapaa linatokomezwa kabisa na kuendelea kuishi kwa upendo, usawa na
amani.

“Uzinduzi
wa leo umeonesha upendo na kujali masuala ya watu wanaoishi na Virusi
vya UKIMWI hiyo niwaombe viongozi wa dini kuungana na jitihada za
mapambano haya kwa kuzitumia nafasi zenu kukemea masuala ya unyanyapaa
kwa watu wanaosihi na maambukizi.

“Viongozi
wa dini tuendelee kuliangalia hili kwa kukemea masuala ya unyanyapaa
kwa malengo ya kuifikia 909090 na ikumbukwe hakuna sababu ya kufanya
hivyo kwa kuzingatia usemi usemao asohili analile,”alisisitiza Leticia.