Waziri mhe. silaa awasili shinyanga na kutoa siku saba kwa katibu mkuu wa wiraza hiyo pamoja na msajili wa mabaraza ya ardhi na nyumba


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya
makazi Mhe.Jerry Silaa ametoa siku saba kwa katibu mkuu wa Wizara hiyo
kushughulikia mgogoro wa ardhi baina ya halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na
Nyang’wale Mkoa wa Geita.

Ametoa agizo hilo leo Jumatatu Disemba
4,2023 wakati akizungumza na baadhi ya viongozi maafisa na watumishi wa idara
ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga
wakiwemo wakuu waWilaya na wabunge kutoka kwenye majimbo ya Mkoa wa Shinyanga.

Waziri Mhe. Silaa kufuatia hoja
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje
kuhusu mgogoro huo, ambapo amemwelekeza  katibu
mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha timu inayoongozwa na wakurugenzi wa upimaji
ramani wanafika na kushughulikia changamoto hiyo.

Katika agizo hilo pia Waziri Mhe. Silaa
amemtaka msajili wa mabaraza ya ardhi na nyumba kufika Mkoani Shinyanga ndani
ya siku saba na kwamba .

“Suala
la mpaka baina ya Nyang’wale na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga naomba
kusema mambo mawili la kwanza na namwelekeza katibu mkuu ndani ya siku saba
kuansia leo ahakikishe timu  inayoongozwa
na wakurugenzi wa upimaji na ramani ifike kwenye mpaka huo lakini  jambo la pili ndani ya siku saba hizo hizo
msajili wa mabaraza ya ardhi na nyumba afike Shinyanga na taarifa zao nizipate
kabla ya terehe 14 Mwezi huu wa kumi na mbili”
.amesema
Waziri Silaa

Aidha Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo
ya makazi Mhe. Jerry Silaa amewataka watumishi wa ardhi kufanyakazi kwa weledi
na kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia taaluma zao.

Kwa upande wake kamishna msaidizi wa ardhi
Mkoa wa Shinyanga Leo Komba amesema Mkoa wa Shinyanga umefanyia kazi maelekezo
yote yaliyotolewa na wizara huku akiahidi kuendelea kushughulikia changamoto
zinazojitokeza.

Mkuu wa idara ya ardhi Wilaya ya Kahama
Clemence Mkusa akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine wa idara hiyo ameahidi
kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na
wizara hiyo.

Waziri Mhe. Silaa amefika Mkoani Shinyanga
kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya baraza la mawaziri kuhusu
utatuzi wa migogoro ya ardhi.

 

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya
makazi Mhe.Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya viongozi maafisa na watumishi
wa idara ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa
Shinyanga wakiwemo wakuu waWilaya na wabunge kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi Mkoa
wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa
maelekezo ya baraza la mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya
makazi Mhe.Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya viongozi maafisa na watumishi
wa idara ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa
Shinyanga wakiwemo wakuu waWilaya na wabunge kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi Mkoa
wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa
maelekezo ya baraza la mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina
mndeme upande wa kulia, katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo
katikati pamoja na mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita upande wa kushoto.

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga
wakiwemo maafisa na watumishi wa idara ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa
Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Waziri wa ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi Mhe.Jerry Silaa, leo Jumatatu Disemba 4,2023 katika ukumbi
wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa idara ya ardhi Wilaya ya Kahama
Clemence Mkusa akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine wa idara hiyo leo
Jumatatu Disemba 4,2023 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga.