WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana na jamii kwa ujumla wasikwepe
jukumu la kuwatunza wazee kwa sababu nguvu zao za uzalishaji mali
zimepungua kutokana na kazi waliyoifanya wakiwa vijana kwa ajili ya
maendeleo na ustawi wa familia zao na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati
wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee uliozinduliwa Januari, 2019
ili kwa kutokomeza ukatili kwa wazee ifikapo 2023 na kuhakikisha wazee
na watu wenye ulemavu wanatambuliwa na kulindwa dhidi ya ubaguzi,
uonevu, ukatili na mila potofu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 29, 2019) wakati
akizindua kambi ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee na watu wenye
ulemavu katika viwanja vya Kichanganimjini Iringa. Kambi hiyo
imeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Ritta Kabati katika
kuadhimisha siku ya Wazee Duniani.

Amesema wajibu wa kuwahudumia au kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu
ni wa kila mmoja na wanapaswa watambue kwamba wazee hao wamelitumikia
Taifa kwa muda mrefu tena kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwaletea na
kuhakikisha wanapata mafanikio hayo ambayo wanajivunia sasa.

“Kwa msingi huo, tunao wajibu wa kuwajali wazee wetu kwa hali na mali
ikiwa ni sehemu ya matunda ya uwajibikaji wao kwetu na kwa Taifa kwa
ujumla. Hivyo basi, tutumie vema Kambi hii kuwasaidia wazee wetu na watu
wenye ulemavu kwa kutambua afya zao na kuwapatia matibabu ya kiafaya
ili waendelee kuwa salama na wenye furaha nasi tuvune busara zao.”

Kutokana na umuhimu wa kuwatunza wazee na kuwasaidia watu wenye ulemavu,
Waziri Mkuu ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wananchi na
wadau mbalimbali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa fursa, haki na
ustawi wa wazee ikiwemo kuondokana kabisa na vitendo vya ukatili dhidi
yao.

“Vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za
haraka kwa wazee wetu wenye vitambulisho. Tengeni dirisha maalumu kwa
ajili ya kuwahudumia ili wasikae kwenye foleni muda mrefu. Serikali
itaendelea kuweka miundombinu na mazingira rafiki ili kuwawezesha kupata
mahitaji yao.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kusimamia maelekezo
yake kwa Halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wasiojiweza na
kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo. “Namshukuru Mbunge wa
Viti Maalum Ritha Kabati amebainisha mafanikio yanayoendelea kupatikana
kutokana na utekelezaji wa agizo hilo.

“Haidhuru nasi tukiiga mfano wa Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti
Maalumu na kaka yangu Mheshimiwa Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu kwa moyo wao
wa kizalendo kabisa kuona kuna haja ya kusaidia na kuunga mkono juhudi
za Rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli za kuwahudumia wanyonge.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini
kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu kwa kuwatambua na kuwapatia
vitambulisho wazee wote nchini wasio na uwezo ili waweze kunufaika na
huduma ya matibabu bila malipo pamoja na huduma zingine za kijamii.

Vilevile, Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Novemba 2019 nchi inatarajia
kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wazee kama sehemu ya jamii wana
haki ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuchagua viongozi wanaoona
watafaa kuwaongoza na wao kuchaguliwa kuongoza katika nafasi mbalimbali.
Hivyo wasaidiwe kushiriki zoezi hilo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) mkoa wa Iringa, Peter Pinda alimpongeza Dkt. Ritta kwa uamuzi wake
wa kuandaa kambi hiyo ambayo itatoa fursa kwa wazee kupima afya zao na
kupatiwa huduma pamoja na kutoa viungo bandia kwa baadhi ya walemavu.

“Uzee ni hali siyokwepeka upende usipende ila unaweza kucheleweshwa
kutegemea na aina ya matunzo wanayopatiwa. Nashauri wazee wapate vyakula
bora tena kwa uwiano sahihi, vyakula hivyo ni pamoja na vya jamii ya
mizizi, mikunde, nafaka, mbogamboga na nyama ili waweze kuimarisha afya
zao.”

Awali, Waziri Mkuu alipokea taariza za ujenzi wa jengo la Ustawi wa
Jamii Manispaa ya Iringa lilojengwa kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa Kundi
la Makampuni ya Asas, Salim Abri kwa gharama ya sh. milioni 60.

Kwa upande wake,Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa Tiniel Mmbaga
alisema kukamilika kwa jengo hilo kutawawezesha kutoa huduma bora kwa
jamii na kwa wakati kwani awali maafisa watano walikuwa wakilundikana
katika chumba kimoja hali iliyosababisha wateja kushindwa kueleza
matatizo yao baada ya kukosekana kwa usiri.

Alisema kwa siku wanashughulikia malalamiko yahusuyo masuala ya migogoro
ya familia ikiwemo matunzo ya watoto kuanzia 15 hadi 30 pamoja na
wanawake zaidi ya 50 ambao kila mwezi wanakwenda kuchukua fedha kwa
ajili ya matunzo ya watoto zinazotolewa na wenza wao kufuatia kuwepo kwa
migogoro baina yao.

Shughuli hiyo, imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Josephat
Kandege, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira
na wenye UlemavuStela Ikupa pamoja na Maafisa wengine wa Serikali.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,