WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini
wasimamie ipasavyo suala la elimu hususani kwa watoto wa kike na
kuchukua hatua kwa watakaowakatisha masomo.

Pia,
Waziri Mkuu amesema Serikali inawataka watoto watoe taarifa za watu
wanaotaka kuwakatisha masomo yao kwa viongozi wa shehiya (vijiji)
waliopo kwenye maeneo yao.

Alitoa
agizo hilo jana jioni (Jumapili, Januari 19, 2020) wakati akizungumza
na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha Mafunzo ya
Amali cha Daya kilichopo Mtambwe wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.

Waziri
Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike lengo likiwa
ni kuhakikisha wanamaliza masomo yao na hatimaye waweze kujikwamua wao
pamoja na familia zao.

Alisema
watoto wa kike wanatakiwa waheshimiwe na jamii kwa kuachwa waendelee na
masomo yao bila ya usumbufu wowote na atakayebainika kukatisha masomo
adhabu yake ni miaka 30 jela.

“Wanafunzi
wa kike hakikisha mtu yeyote atakayekugusa, kukufuatilia nenda
kamshtaki kwa kiongozi wa Shehiya husika. Vijana jihadharini na watoto
wa shule ukikutwa naye jela miaka 30.”

Awali,
akisoma taarifa za ujenzi wa chuo hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bibi Madina Abdallah alisema mpaka
kukamilika kwake mradi huo utagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni
25.8 kati yake Dola milioni 23.4 zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) huku dola milioni 2.4 zikitolewa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.

kwa mujibu wa mkataba wa mradi huo kazi ya ujenzi inajumuisha vituo
viwili vya Mafunzo ya Amali ambavyo ni Makunduchi Unguja na Daya Pemba.
Pia upanuzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Utalii Maruhubi na Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia ya Karume pamoja na ununuzi wa vifaa vya
kufundishia.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU