Waziri mkuu kassim majaliwa azindua jengo la ofisi ya halmashauri ya mbinga

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 4, 2021 amezindua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Mkoani Ruvuma.

Pia, Waziri Mkuu alikagua nyumba 7 za Wakuu wa Idara za  Halmashauri ya Mji wa Mbinga zilizojengwa  na Serikali kwa gharama ya sh. Milioni 321.771.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Grace Quintine amesema lengo la miradi hii ni kuboresha mazingira ya makazi ya watumishi wa halmashauri ikiwa ni pamoja na kupunguza kilipa posho za nyumba kwa kila mwezi

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda ahakikishe anawakamata viongozi wa AMCOS kwa tuhuma za kutoa fedha za wanachama na kuwapa madiwani ili wakawashawishi madiwani wenzao wakubali kubadilisha eneo la ujenzi wa ofosi za Halmashauri ya Wilaya hiyo.

 

Madiwani waliohusika katika mvutano huo ni wa kata za Mkumbi (Bruno Kapinga), kata ya Lukalasi (Bosco Ndimbo) na wa kata ya Linda (Haule), ambao wanadaiwa kuchukua fedha kutoka kwa watendaji wa AMCOS kwa ajili ya kwenda kushawishi madiwani wenzao wakubali kuhamishwa kwa eneo la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.