Waziri mkuu majaliwa kufungua maonyesho ya sido singida oktoba 4, 2019

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu
mkoani Singida na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.


Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa jana Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt.Rehema Nchimbi alisema ziara hiyo ataianza Oktoba 4, 2019 na Oktoba 7
atafungua rasmi maonesho ya pili ya viwanda vidogo vidogo (SIDO)
yatakayofanyika kitaifa mkoani humo.

NCHI
sita za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC) zinatarajiwa kushiriki
maonesho hayo ambazo ni Kenya, Burundi, Ruanda, Uganda, China, India na
Afrika kusini.

Dkt.Nchimbi
alisema maonesho hayo yataanza kufanyika Oktoba 4 hadi 9 mwaka huu,na
yatafunguliwa rasmi oktoba 7 na waziri mkuu Kassimu Majaliwa.


Maonesho haya yatafanyika sanjari na maadhimisho ya wiki ya chakula
duniani ambayo yatafanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 16 mwaka huu katika
Viwanja vya Bombadier zamani Peoples” alisema Nchimbi.

Alisema
kufanyika maonesho hayo mkoani Singida ni fursa kwa wananchi wa mkoa
huo ambao unakuwa kiuchumi kutokana na shughuli za kilimo, ufugaji,
biashara na viwanda.

Pia
alisema mkoa wa Singida wanajivunia kuchaguliwa kufanyika kwa maonesho
hayo kitaifa na hii itawapa hamasa kubwa wananchi katika kuanzisha
viwanda vidogo vidogo vya usindikaji kutokana na mazao yanayolimwa
mkoani hapa.

Dkt.
Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa mkoa huo na
mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kupokea ugeni huo na kushiriki
katika maonesho hayo.

Aidha
mkuu wa mkoa alisema kabla ya kufungua maonesho hayo waziri mkuu Kassim
Majaliwa atafanya ziara ya kikazi kila wilaya na halmashauri zote za
mkoa huo na kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi katika mkutano wa
hadhara.

Katika
ziara hiyo Majaliwa atatembelea miradi mbalimbali ya kimkoa na miradi
mikubwa ya kitaifa, ambapo miradi ya kitaifa ni mradi wa kupokea na
kupozea umeme uliopo katika halmashauri ya manispaa ya Singida pamoja na
mradi wa daraja Sibiti linalounganisha mkoa wa Singida na Simiyu
lililopo wilayani
Mkalama.