Waziri mpina azindua vituo vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo sumbawanga

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akizindua  kwa
pamoja vituo viwili vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC) na Wakala
wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Kanda ya Magharibi- Sumbawanga
jana. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara Tanzania (TVLA),
Dk. Furaha Mramba na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania,
Maghembe Makoye
 
NA MWANDISHI WETU, RUKWA
WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua kwa pamoja vituo viwili vya
Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC) na Wakala wa Maabara ya Veterinari
Tanzania (TVLA) Kanda ya Magharibi- Sumbawanga na kutangaza msimamo wa
Serikali ya awamu ya tano wa kupambana na magonjwa ya mifugo ili
kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake nchini.
Hivyo
Serikali inawahakikishia wananchi uhakika wa upatikanaji wa chanjo kwa
bei nafuu kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanyika ikiwa ni pamoja na
Taasisi ya Chanjo (TVI) kuzalisha chanjo za kimkakati 11 ifikapo Juni
mwakani na kwamba Serikali iko mbioni kutangaza bei elekezi ya Chanjo
ili kuwadhibiti watu wachache waliokuwa wanawaibia wananchi.

Aliongeza
kuwa hivi sasa kuna ujenzi mkubwa wa Kiwanda kipya cha kuzalisha chanjo
cha Hester Bioscience Africa Limited (HBAL) ambacho kitazalisha chanjo
27 ifikapo Juni na uwekezaji wake una thamani ya zaidi ya Shilingi
bilioni 50 na kuwezesha upatikanaji wa chanjo zote kwa wafugaji wa ndani
ya nchi, Afrika na Dunia.
Akizungumza
mara baada ya kuzindua vituo hivyo vitakachohudumia mikoa ya Songwe,
Rukwa na Katavi vyenye makao yake mjini Sumbawanga, Waziri Mpina amesema
kamwe Serikali haiwezi kukubali mifugo iendelee kufa kwa magonjwa na
kwamba sasa magonjwa hayo hayana nafasi tena nchini.
Hivyo
Serikali imeamua kuandaa Kanuni mpya za usimamizi wa uogeshaji na
uchanjaji mifugo ili kudhibiti utoaji wa chanjo kwa wananchi na kwamba
itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote wataokwenda kinyume
na kanuni hizo.
Hivyo
ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinashirikiana kwa
karibu na vituo vya uchunguzi wa magonjwa na wakala wa maabara ya
magonjwa ya mifugo vilivyoko katika kanda zao ili kutoa huduma bora kwa
wafugaji na kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake.
Waziri
Mpina pia amemuagiza Katibu Mkuu Mifugo na Katibu Mkuu Tamisemi kufanya
mgawanyo mpya wa maafisa mifugo ili kuweza kupelekwa kwenye maeneo
ambayo hayana kabisa maafisa mifugo ukiwemo Mkoa wa Katavi ambao hauna
kabisa Madaktari wa Mifugo.
Pia
ameagiza ZVC na TVLA Kanda ya Magharibi Sumbawanga kuwa wasimamizi na
walezi wazuri wa wafugaji na mifugo na kuhakikisha kuwa chanjo,
uogeshaji na haki za mifugo zinasimamiwa kikamilifu.
Waziri
Mpina pia ameiagiza Kanda kusimamia kikamilifu uingizaji wa chanjo,
madawa, viuatilifu, chakula na mazao ya mifugo yanayoingizwa nchini bila
vibali, bila kulipiwa ushuru, bila kukaguliwa na yaliyokwisha muda wa
matumizi na feki.
Kufuatia
mageuzi ya utoaji huduma za mifugo nchini, Waziri Mpina amemwagiza
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kufanya ukaguzi wa maafisa wa kanda zote
ili kupanga safu mpya itakayokuwa tayari kuendana na kasi ya Serikali ya
awamu ya tano.
Waziri
Mpina ameonya kuwa siku nyingine ikitokea hatua zikachelewa kuchukuliwa
kwa maafisa  wanaohujumu mifugo basi Mkurugenzi wa huduma za mifugo
ataondolewa kwenye wadhifa wake.
Waziri
Mpina alisema wafugaji walikuwa wakipata huduma za uchunguzi wa
magonjwa kilichopo Iringa umbali wa zaidi ya kilomita 900 kutoka
Sumbawanga  hali ilisababisha ugumu kwa wafugaji na kusababisha vifo
vingi vya mifugo
Hivyo
Waziri Mpina amebanisha kuwa uanzishaji wa kanda hiyo utaongeza ufanisi
wa kazi ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo katika mikoa ya Songwe, Rukwa
na Katavi na kuleta ahueni kubwa kwa wafugaji.
Mpina
aliongeza kuwa hadi sasa kuna Kanda 8 za Uchunguzi wa Magonjwa ya
Mifugo na Kanda 11 za Wakala wa Maabara Tanzania (TVLA) ambapo wizara
inakusudia kuanzisha kanda nyingine moja katika mwaka fedha wa 2019/
2020 itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kituo hicho
kikikamilika kitasogeza huduma ya udhibiti wa magonjwa katika mikoa
hiyo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Mifugo nchini, Dk Hezron Nonga amesema tangu kuanzishwa
kwa kituo hicho kumewezesha kuongezeka kwa huduma za uchunguzi wa
magonjwa ya mifugo na mazao yake, shughuli za uchunguzi kimaabara
zimesogezwa karibu na wananchi.
Pia
upatikanaji wa chanjo kwa wafugaji kwa bei nafuu umekuwa rahisi,
kuongezeka kwa upatikanaji wa taarifa za magonjwa , kuongezeka kwa
majosho hamasa ya wafugaji kuongeza mifugo na idadi ya lita za kuogesha
mifugo.
Pia
ongezeko la maduhuli ya Serikali yatokanayo na usafirishaji wa mifugo
na mazao yake ndani na nje ya nchi kutoka makadirio ya sh milioni 120
kwa mikoa miwili Rukwa na Katavi hapo awali na kufikia makadirio ya  sh
milioni 500 kwa mwaka, kufanikiwa kudhibiti ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Dk
Nonga amesema pia kumeongezeka mahusiano kati ya wizara na Serikali za
mitaa na hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za mifugo kwa
wananchi tofauti na ilivyokuwa awali.