Waziri ndaki azindua mwongozo wa utoaji wa chanjo za mifugo nchini,asema utalinda afya ya mnyama

 

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza kwenye hafla ya
uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa
mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika
jijini Dodoma Januari 22,2021.



Baadhi
ya wadau wa Sekta ya Mifugo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa
Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa
ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma
Januari 22,2021.



Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul,akizungumza kwenye hafla
ya uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo
kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika
jijini Dodoma Januari 22,2021.



Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo prof. Elisante
Ole Gabriel,akisisitiza jambo kwa wadau wa sekta ya mifugo (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya
magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na
binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.



Mkuu
wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma kwenye uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa
ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi
iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.



Mkuu
wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri ,akitoa maoni kwa niaba ya
wakuu wa wilaya zote za Dodoma wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa
utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano
kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari
22,2021.




Mtaalamu wa kufuatilia Magonjwa ya Mifugo FAO Dkt.Niwael Mtui
akiwaelezea wadau wa sekta ya mifugo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa
utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano
kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari
22,2021.



Muwakilisha
wa wataalamu wa mifugo Wastaafu Tanzania (UWAMIWATA) akichagia wakati
wa uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo
kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika
jijini Dodoma Januari 22,2021.




Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt.Omary Nkullo
akizungumza kwenye uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya
magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na
binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.




Baadhi ya wadau wa Sekta ya Mifugo wakifatilia Uzinduzi wa Mwongozo wa
utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano
kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari
22,2021.




Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa
mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika
jijini Dodoma Januari 22,2021.



Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Naibu Waziri wa
wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya
magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla
fupi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.



Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya
Bahi Mhe. Mwanahamisi Mukunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge, mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya
mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla iliyofanyika
jijini Dodoma Januari 2.2021.



Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya
Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri,mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya
magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla
iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.



Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa Dk.Suleiman Serera,mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa
ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla
iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.



Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama
cha Wafugaji nchini Bw. Jeremiah Wambura mwongozo wa utoaji wa chanjo
dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika
hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.




Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini Bw. Jeremiah Wambura akitoa
neno la shukrani kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki mara
baada ya kuzindua mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya
mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla fupi
iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.



Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kuzindua mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya
mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla fupi
iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.


……………………………………………………………………………………….


Na.Alex Sonna,Dodoma


Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki amezindua mwongozo wa utoaji wa
chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini, wenye lengo la kuhakikisha
sekta binafsi na umma zinajua haki na wajibu katika zoezi zima la utoaji
wa chanjo na kuhakikisha afya ya mnyama inabaki salama.


Mara
baada ya kuzindua mwongozo huo jijini Dodoma Januari 22,2021 Mhe.Ndaki
aameagiza kusimamishwa kwa muda, utoaji wa chanjo unaofanywa na
halmashauri nchini kupitia kampuni walizoingia nazo mikataba, baada ya
kubaini chanjo kutolewa kiholela kwa mifugo bila kuwepo utaratibu sahihi
na kusababisha madhara kwa mifugo na hasara kwa mfugaji.


Aidha
Mhe.Ndaki amesema kuwa katika kuhakikisha mwongozo wa utoaji wa chanjo
dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini, unakuwa na tija kwa taifa hivyo
nataka haki na wajibu kwa kila wadau wa mifugo.


“Hapa
tunaangalia afya ya mifugo, afya ya mifugo ilikuwa hatarini ni kweli
utaratibu wanafanya halmashauri lakini hauko wazi sana, ndiyo maana
tukasema sasa ni muhimu kuwa na mwongozo huu kutuelekeza nini cha
kufanya, chanjo ikifanywa vizuri kwa usahihi bila makosa tuliyokuwa
tunayaona tunaweza kuwa na ng’ombe wenye afya bora na njema.” Amesema
Mhe.Ndaki


Aidha,
amesema kuwa mwongozo huo umeshirikisha wadau zaidi ya thelathini
wakati wa kuundaa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo tayari kupokea maoni ya
wadau sehemu ambazo mwongozo utaonekana kuwa na mapungufu ili
kuurekebisha na kuufanya uwe bora zaidi, lengo likiwa ni kuhakikisha
afya ya mifugo nchini inalindwa na mfugaji kutopata hasara ya mifugo
yake kufa au kupata madhara mengine yoyote baada ya kuchanjwa.


Hata
hivyo Mhe Ndaki amesema kuwa wizara itahakikisha inaandaa mazingira
mazuri ya kuwa pamoja na sekta binafsi ili kufanya kazi pamoja ambayo
itakuwa na tija kwa taifa na wafugaji kwa ujumla.


“Sekta
binafsi nipende kuwahakikishieni kuwa sisi tutafanya kazi na sekta
binafsi vizuri kabisa tusiwe na mashaka ni vile tuliona kasoro, lakini
niwaombeni sekta binafsi hasa wale mlio vizuri katika jambo hili la
chanjo msiwe na wasiwasi hata mkiingia mikataba na halmashauri ili mradi
muwe na sifa na vigezo ndiyo maana ya sisi tukatoa mwongozo ili tufanye
kazi pamoja.” Amefafanua Mhe.Ndaki


Hata
hivyo Waziri Ndaki amewataka viongozi wenzake wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, mamlaka za serikali za mitaa, watoa huduma za afya ya mifugo na
sekretarieti za mikoa wazingatie maelekezo yaliyopo kwenye mwongozo wa
utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini na kutoa maoni au
kuuliza maswali sehemu ambazo zitakuwa na utata ili kuhakikisha mwongozo
huo unatekelezwa kama ambavyo umezingatiwa kwa ajili ya kudhibiti
magonjwa ya mifugo nchini.


Ameitaka
pia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa nakala za kutosha za mwongozo huo
kwa wadau wa sekta ya mifugo kote nchini na pia kuwataka wadau kupata
nakala laini kupitia tovuti ya wizara hiyo, www.mifugouvuvi.go.tz.


Awali
akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mkuu wa
Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Mukunda amesema kuwa mkoa huo
utahakikisha yale yote ambayo Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatamani
yatokee katika Sekta ya Mifugo mkoa upo tayari kuyasimamia ili yalete
tija kwa taifa na wafugaji.


“Ili
pia mwongozo huu uweze kufanya vizuri kama ya wataalamu wa mifugo bado
haitoshi hivyo ni vyema wataalamu waliopo katika ngazi za juu waweze
kuwafikia pia wafugaji wa chini na tunataka kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa
kitovu cha kuzalisha nyama na maziwa kwa wingi.” Amesema Mhe.Mukunda


Mhe.Mukunda
amesema kuwa Sekta ya Mifugo kwa sasa imekuwa ikirasimishwa rasmi na
kuifanya iheshimishe watu wanaofanya shughuli za mifugo kwa kuwa imekuwa
na tija kubwa kwa taifa na mtu mmoja mmoja.


Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul amesema
kuwa serikali bado inahakikisha inafanya jitihada mbalimbali za kupata
masoko zaidi ya mazao ya mifugo yenye ubora ambayo yanachochewa na uwepo
wa chanjo bora na mifugo.


“Wenzangu
niwaombe mpokee huu waraka ulipo ukatusaidie ili malalamiko ya mnada
umeharibika au wilaya nzima kutokuwa na josho, hayo malalamiko yafike
mwisho kupitia mapato mbalimbali ambayo halmashauri wamekuwa wakipata
yakiwemo ya minada iliyopo kwenye wilaya hizo, wanapaswa kutenga fedha
kwa ajili ya kuyakarabati.” Amefafanua Mhe. Gekul


Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini Bw. Jeremiah Wambura amesema
kuwa tasnia ya maziwa nchini ikisimamiwa vyema inaweza kuongeza kwa
kiasi kikubwa pato la taifa na kuhamasisha uwepo wa viwanda vingi vya
kuchakata maziwa nchini.


Hivyo
ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuangalia vyema namna ya kuisimamia
tasnia ya maziwa ili iwe na tija zaidi kwa taifa pamoja na kuongeza
wingi wa maziwa ambayo yanaweza kutumika majumbani pamoja na kuchakatwa
viwandani.


Mara
baada ya uzinduzi wa mwongozo huo Mhe. Ndaki amesema kuwa kuanzia sasa
mwongozo huo unaweza kutumika na huduma ya chanjo kuendelea kutolewa na
sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali.