Waziri ummy atoa agizo kwa wanaoendelea kutumia vifungashio

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ziara yake
ya siku moja mkoani Tanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ziara yake
ya siku moja mkoani Tanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza Katibu Tawala
wa Mkoa wa Tanga Judica Omari kushoto wakati wa ziara hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo

WAZIRI
wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu kushoto akiteta
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara hiyo


WAZIRI wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ameagiza watu ambao
watabainika kutumia vifungashio vya mifuko ya Plastic baada ya miezi mitatu
aliyoitoa kupita wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Ummy alitoa agizo
hilo wakati wa ziara yake katika Jiji la Tanga kubwa ni kutokana na malalamiko
yanayotoka kwenye Jiji hilo kuhusu uchafuzi wa mazingira unaotokana na viwanda
vilivyopo vya kuzalisha saruji na chokaa.


Alisema kwamba suala
la vifungashio alikwisha kutoa miezi mitatu ambapo mwezi Aprili mwaka huu ndio
litakuwa limekwisha hivyo hategemei kuona baada ya kumalizika watu wataendelea
kutumia vifungashio vya namna hiyo.


“Nisisitize suala la
vifungashio nilitoa miezi mitatu mwezi wanne litakuwa limekwisha baada ya miezi
mitatu kwisha tutatoa agizo la kuwaambia mkamatwe kwa yeyote ambaye anatumia
vifungashio maana mifuko ya plastic imerudi kwa kigezo cha vifungashio”Alisema Waziri
Ummy.


Aidha alisema kwamba
hivi sasa unaona watu wameweka karoti wamezifunga kwenye mifuko kwamba wamerudisha
mifuko ya plastic kwa  kigezo cha
vifungashio hivyo endele kuzibidi mifuko hiyo.


“Lakini ikiisha miezi
mitatu niliyoitoa mtakayemkuta anaendelea kutumia mifuko ya plastic endeleeni
kuchukua hatua stahiki dhidi yao “Alisema .

Hata hivyo Waziri Ummy
alizitaka Halmashauri ziandae mpango kazi wa Mazingira ambao utakuwa na tija
kubwa katika kusimamia na utekelezaji wa kazi hizo kwenye maeneo yao.

Alisema mpango huo
lazima utengewe bajeti kwa sababu ni suala muhimu kama yalivyo masuala mengine
ambayo yamekuwa yakifanyiwa hivyo katika maeneo husika.


“Pia tuhakikishe Halamshauri
zote zinaweka vipaumbele na bajeti ya kutekeleza shughuli za utunzaji na
uhifadhi mazingira lakini pia suala la uteuzi wa maafisa mazingira kwenye
mamlaka ya serikali za mitaa waendelee nalo”Alisema


Waziri Ummy Ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga alisema lakini changamoto zilizopo bado hakuna
mfumo mzuri wa ngazi ya halmashauri ya Usimamizi wa shughuli za Mazingira.


Kutokana na uwepo wa
changamoto hiyo Waziri Ummy alimuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Kukaa na Katibu Mkuu Tamisemi ili kutengeneza mfumo mzuri .


Alisema kwa sababu
wanaweze kuwa wanapiga kelele mkoani lakini kama Halmashauri hazitakuwa na
mfumo nzuri wa kusimamia shughuli za mazingira hataweza kupata hayo matokeo
ambayo wameyapata ili tufanikishe lazima warekebishe muundo kwenye ngazi ya
Halamshauri za Serikali za Mitaa.


Awali akizungumza
wakati wa ziara hiyo,Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Thimotheo Sosiya alisema
mkoa huu unatekeleza kampeni ya mazingira kwa pamoja kila Jumamosi ya mwisho wa
mwezi na imeleta mafanikio makubwa kwenye kutkomeza uchafuzi maeneo korofi na
mazingira.


Aisema lakini katika
suala hilo changamoto kubwa ni uwezo mdogo wa Halmashauri kuondosha taka ngumu ikiwemo
mwitiko mdogo wananchi kufanya usafi kwa hiari huku akieleza mkoa umejipanga.


Alisema kujipanga
huko ni kuunda vikosi kazi kwenye Halmashauri ambavyo vitakuwa na kazi ya
kusimamia mazingira na kwamba wanaotupa taka sasa wawepo watu ambao wanakuwa tayari
kuwakamata na kuwapiga faini.