Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele wakati wa ziara kwenye mradi wa maji wa Nyahiti |
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akielekeza jambo wakati wa ziara yake kwenye mradi wa maji wa Nyahiti, Wilayani Misungwi |
UONGOZI
wa Wizara ya Maji ukiongozwa na Naibu Waziri, Jumaa Aweso na Naibu
Katibu Mkuu, Mhandisi Anthony Sanga umeweka kambi Wilayani Misungwi kwa
lengo la kupata ufumbuzi wa miradi ya maji inayotekelezwa kwa kusuasua
wilayani humo.

Uamuzi
huo umefikiwa wakati wa ziara ya viongozi hao Desema 3, 2019 ya kukagua
miradi ya maji inayotekelezwa Wilayani Misungwi ambapo walionyesha
kutoridhishwa na hali ya utekelezaji wake.

Akizungumza
juu ya uamuzi huo wa kuweka kambi wilayani humo, Jumaa Aweso alisema
hali aliyoishuhudia ya utekelezaji wa miradi ya maji unakwenda kinyume
na dhamira ya Rais John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wananchi
wanaondokana na kero hiyo haraka iwezekanavyo.

Wakati
wa ziara hiyo, Aweso na Naibu Katibu Mkuu Sanga walikuta ujenzi wa
mradi wa Ihelele na Mbarika unaotekelezwa na Mkandarasi Shanxi
Construction Engineering Corporation ya China ukiwa umesimama kwa madai
ya kuchelewa kufika kwa mabomba ya chuma (steel pipes) kutoka kwa mtoa
huduma kiwanda cha Tanzania Steel Pipe (TSP) jambo ambalo liliwalazimu
kuitisha kikao cha dharura kitakachohusisha wadau wanaohusika na ujenzi
wa mradi.

“Hili
suala halikubaliki, Serikali imetoa fedha lakini hakuna kinachoendelea,
ninaagiza kesho nikutane na TSP, Mkandarasi na Msimamizi wa mradi
KASHWASA ili tupate ufumbuzi wa pamoja,” alisisitiza Naibu Waziri
Aweso.

Aweso
alisisitiza kuwa hatoondoka Wilayani humo hadi hapo utatuzi wa bomba
hizo utakapopatikana ikiwa ni pamoja na TSP kuthibitisha lini
watakamilisha na kuleta mabomba hayo.

“Nimeelezwa
kwamba TSP bado inadai kiasi cha fedha ili kukamilisha mabomba,
niwathibitishie wananchi wa Misungwi Rais Dkt. John Pombe Magufuli
ametupatia fedha sasa tunataka kiwanda kituthibitishie lini
kitakamilisha mabomba haya ya mradi,” alisema Aweso.

Mbali na hilo, Aweso alimuagiza Mkandarasi kuhakikisha ifikapo Machi, 2020 mradi uwe umekamilika na wananchi wanapata huduma
Kwa
upande wake Mhandisi Sanga alisisitiza kuwa fedha za kutekeza miradi ya
maji Wilayani Misungwi ilikwishatengwa na alisisitiza Mkandarasi
kuhakikisha anakamilisha kazi kama alivyoelekezwa.

Mhandisi
Sanga alishukuru jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika
kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero ya maji ambapo alisema fedha
imekuwa ikitoka kwa wakati na hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha
miradi.

“Namshukuru
sana Mhe. Rais kwani hajawahi kuchelewa kutupatia fedha ya kukamilisha
miradi na amekuwa mstari wa mbele kufuatilia na kila anapoahidi hajaacha
kutekeleza,” alisema Mhandisi Sanga.

Mradi wa Maji Ihelele utanufaisha zaidi ya wananchi 81,000 kutoka vijiji vya Nyang’omango, Isesa, Igenge na Mbarika.