Kaimu Mkurugenzi wa
Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni akizungumza
na wananchi wa kata ya Makuyuni kuhusu jitihada za Serikali za
kukabiliana na tatizo la wanyamapori kuvamia makazi ya watu nchini,
katika kikao kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.
Diwani wa Kata ya
Makuyuni, Elias Odupoi akiwatambulisha Watendaji kutoka Wizara ya
Maliasili na Utalii na Taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao na
wananchi cha kutatua tatizo la tembo kuvamia makazi ya watu kwenye kata
yake kilichofanyika leo.
Wananchi wa Kata ya
Makuyuni wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao kuhusu jitihada za Serikali za kukabiliana na tatizo la
wanyamapori kuvamia makazi ya watu nchini, katika kikao kilichofanyika
kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.
Mkazi wa Kata ya
Makuyuni, Kakesyo Lucas akielezea tatizo la tembo kuvamia makazi yao
katika kikao cha wananchi na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.
Mkazi wa Kata ya
Makuyuni, Thobias Laiza (kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi wa
Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni (kulia)
picha ya vipimo vya Xray vya mtoto wake aliyejeruhiwa na tembo
katika kikao cha wananchi na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.
Kaimu Mkurugenzi wa
Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni (kushoto)
akiteta jambo na Mwandishi wa ITV/RADIO ONE, Asiraji Mvungi mara baada
ya kikao cha wananchi na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.