Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akifafanua jambo
kwenye mkutano wa mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani
Morogoro.JPGNaibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akifafanua jambo kwenye mkutano
wa mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani Morogoro.

Baadhi ya wajumbe walioshiriki
kwenye mkutano wa mashaurinao kati ya serikali na wawekezaji Mkoani
Morogoro ambapo walipewa fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao

Picha ya pamoja ya baadhi ya
mawaziri na naibu mawaziri walioshiriki kwenye mkutano wa mashauriano
kati ya serikali na wawekezaji Mkoani Morogoro

Na. Edward Kondela
Wizara ya Mifugo
na Uvuvi imepongezwa kwa kuwa moja ya wizara ambazo ni vinara katika
kusimamia na kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano kuelekea
uchumi wa kati unaotegemea viwanda kwa kusimamia uanzishwaji wa viwanda
vinavyotegemea malighafi za mifugo.

Akizungumza jana
(04.12.2019) kwenye mkutano wa mashauriano kati ya serikali na
wawekezaji Mkoani Morogoro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki, amesema uanzishwaji wa viwanda vya
kusindika maziwa ni moja ya vipaumbele katika ofisi ya waziri mkuu jambo
ambalo limekuwa likisimamiwa vyema na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo
viwanda kadhaa vimeanzishwa na vingine vinaendelea kuanzishwa vikiwemo
vya kuchakata ngozi.

Mhe. Kairuki
ambaye ni mwenyekiti wa mikutano hiyo inayofanyika katika mikoa ya
Morogoro, Pwani na Dar es Salaam ikishirikisha wizara 13 wakiwemo
mawaziri na naibu mawaziri amesema wizara yake itahakikisha inaendelea
kushirikiana na wizara nyingine katika kuweka mazingira bora zaidi ya
wawekezaji ili kuanzishwa kwa viwanda vingi zaidi hali ambayo itakuza
uchumi wa nchi na wananchi.

Awali akizungumza
kwenye mkutano huo Mkoani Morogoro kuhusu sekta ya mifugo, Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema wizara tayari imeanza
matumizi ya mizani katika minada ya mpakani na upili ili wafugaji waweze
kuuza mifugo yao kwa kupimwa uzito badala ya kukadiria hali ambayo
imekuwa ikiwafanya wafugaji kutopata faida kulingana na muda na gharama
ambazo wanatumia kutunza mifugo yao.

“Tayari
tumeanzisha hili sasa wafugaji wanauza mifugo yao kwa kupimwa uzito,
tunataka tufike mahali baada ya kuwa na mizani ni kuwa na bei ya nyama
kwa kilogramu ili mfugaji aweze kupata faida kwa kuuza mfugo wake,
badala ya kuuza kwa kukadiria wakati mfugaji anahangaika zaidi ya miaka
minne hadi mitano kutunza mfugo wake.” Amesema Mhe. Ulega

Mhe. Ulega
amesema kuhusu maeneo ya malisho ya mifugo, wizara inaboresha sheria ili
ardhi iliyotengwa kwa ajili ya ufugaji na malisho ilindwe na sheria
isiwe rahisi ardhi hiyo kubadilishwa matumizi mengine.

Aidha amefafanua
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli
amefanya jambo kubwa kwa kutoa maelekezo ya kutazamwa maeneo nchini
ambayo yanaweza kutumika kwa ajili ya ufugaji na kilimo, ambapo wizara
kupitia maeneo ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imetoa kiasi
kikubwa maeneo ya malisho kwa wafugaji wanaoweza kukodi kwa muda mfupi
ili mifugo yao iweze kupata maeneo ya malisho ya uhakika.

Naibu waziri huyo
ametoa rai kwa wafugaji na wizara kushirikiana ili kuhakikisha viwanda
vya kusindika maziwa kutozalisha bidhaa chini ya malengo yao kutokana na
uhaba wa maziwa kutoka kwa wafugaji kwa kuwa ushirikiano huo
utaiwezesha wizara kuyafikia masoko na kuwawezesha wafugaji kupata
huduma ya kuweza kufanya shughuli zao na kusisitiza wafugaji wa Mkoa wa
Morogoro kujiunga katika ushirika.

“Kiwanda cha
Tanga Fresh kimefanikiwa kwa kuwa kina ushirika na kinamilikiwa na Chama
Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga
(TDCU) ambacho kina hisa zaidi ya asilimia 40 katika kiwanda hicho
wafugaji wa hapa Mkoani Morogoro nanyi pia mjiunge katika ushirika na
viwanda vya hapa visikose malighafi ya maziwa kwa ajili ya kusindika.” Amesema Mhe. Ulega

Kuhusu
uanzishwaji wa viwanda nchini vinavyotegemea malighafi ya mifugo Naibu
Waziri Ulega amesema kuna takriban viwanda vitano vya kuchakata nyama
vinavyojengwa nchini nzima na kwamba uwepo wa viwanda hivyo vitachangia
matumizi sahihi ya reli ya kisasa (SGR) kwa kuwa utakuwepo utaratibu wa
reli ya mizigo ambapo pia mifugo itasafirishwa na kuwataka wananchi
kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kutumia fursa
zilizopo.

Katika kudhibiti
magonjwa ya mifugo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumza kwenye
mkutano huo wa mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani
Morogoro, amefafanua kuwa serikali imefanya kazi kubwa katika madawa
ambapo Kituo cha Kuzalisha Chanjo Tanzania (TVI) katika kipindi cha
miaka minne kimeweza kubaini magonjwa 11 ya kipaumbele ambapo tayari
chanjo sita ikiwemo ya ugonjwa wa mdondo ambao umekuwa ukiathiri
wafugaji wa kuku tayari zinazalishwa na kupatikana kote nchini.

Amebainisha pia
serikali ya awamu ya tano kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019 imetoa dawa
ya ruzuku kwa majosho yote yanayofanya kazi nchini nzima na mwaka huu
2019/2020 imeendelea kutoa ili mifugo iweze kuogeshwa kudhibiti magonjwa
na kufafanua kuwa mkakati wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kufanya
ukaguzi wa kila mara kubaini ubora wa dawa za mifugo zilizopo madukani
na kwamba itakuwa inadhibiti dawa ili wafugaji wasiendelee kuuziwa dawa
zisizo sahihi na ambazo hazifai kwa matumizi ya mifugo yao.

Katika sekta ya
uvuvi naibu waziri huyo amesema serikali ina kituo cha muda mrefu cha
Kingolwira kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kinazalisha vifaranga vya
samaki ambao wanapatikana kwa bei nafuu zikiwemo pia huduma za
kitaalamu, hivyo kuwataka wananchi kukitumia kituo hicho ili kukuza
uchumi wao kwa kufuga samaki kwa kuwa Tanzania inazalisha samaki Tani
350,000 hadi 400,000 lakini mahitaji ni Tani 800,000 kwa mwaka.

“Sasa hivi
tumeweka mkakati mkubwa wa kuzuia samaki kutoka nje ya nchi ili wananchi
waweze kuchangamkia fursa katika sekta ya uvuvi kwa kufuga samaki na
kufidia soko lililopelea la Tani 400,000 hivyo ni vyema mchangamkie
fursa hii.” Amesema Mhe. Ulega

Kufuatia migogoro
ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ambayo ilijitokeza miaka
iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mhe. Mohamed Utaly
amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa migogoro ya namna hiyo imeisha
katika wilaya hiyo kutokana na juhudi mbalimbali ambazo zimefanywa na
serikali kwa kushirikiana na wananchi.

Mkutano wa
mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani Morogoro, ambao
ulikuwa chini ya mwenyekiti Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki, umehudhuriwa na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Mendeleo Mhe. William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege,

Weninge ni Naibu Waziri wa
Madini Mhe. Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima, Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii Mhe. Costantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira
Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.

Mkutano huo
umehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare pamoja
na watendaji kutoka taasisi na mashirika yaliyo chini ya wizara hizo
pamoja na wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro.