Zaidi ya mifuko mbadala 1400 isiyokuwa na viwango yakamatwa njombe

Na Amiri kilagalila-Njombe

Baraza
la taifa la hifadhi ya mazingira NEMC kanda ya nyanda za juu kusini
wamefanya oparesheni mjini Njombe na kukamata vifungashio zaidi ya 1400
visivyokidhi ubora wa soko katika maduka mbalimbali ya wafanyabiashara.

Katika
oparesheni hiyo mifuko mbadala ambayo haina nembo ya ubora TBS na
maelezo ya ubora wa mfuko pamoja na mifuko ya plastiki inayotumika
kufungashia nyama mabuchani,karanga na hata mahindi ya kukaangwa
imekamatwa .

Baadhi
ya wafanyabiashara waliokamatwa akiwemo Afla Sanga na Anitha Mgaya,
wamekiri kufahamu kuwa wamekiuka sheria na wengine wamedai kuwa  hawajui
chochote kwa kuwa wengine sio wamiliki wa maduka bali ni wafanyakazi.

“Kwa
mimi elimu hiyo sikuwa nayo,kwasabau unajikuta umeenda kununua mfuko wa
kifungashio unafika pale unachukuwa mfuko unaoonekana sokoni na kuja
kuuza”alisema Afla Sanga

Kwa
niaba ya afisa mtendaji wa mtaa wa kwivaha uliopo mjini Njombe mjumbe
wa mtaa huo  bwana Willy Kiswaga anasema sheria zichukue mkondo wake kwa
kuwa mifuko hiyo ilishapigwa marufuku.

Milton
Mponda ni afisa mazingira kutoka NEMC  kanda ya nyanda za juu kusini
amesema zoezi la kukamata na kutaifisha mifuko hiyo ni endelevu huku
akitoa wito kwa wafanyabiashara kujiepusha na uuzaji wa vifungashio feki
kwa kuwa faini yake ni jela miezi mitatu au faini ya kuanzia shilingi
laki moja hadi laki tano kutegemeana na wingi wa mzigo.

“Mpaka
sasa tumekamata pisi sio chini ya 1500,mingi tumekamata kwasababu
haiikidhi viwango,na ile iliyokidhi tumeacha tumeacha waendelee ktumia
na ndio inayoruhusiwa kisheria”alisema Milton Mponda

Mponda
amesema mfuko mbadala ni lazima uwe na taarifa za mzalishaji pamoja na
nembo ya TBS kwa maana ya kukidhi viwango vya TBS VSM 70 pamoja na
kuonyesha uwezo wa mfuko kubeba mzigo