Bonanza la wananchi wa tarafa ya elerai lafana

Uzinduzi wa Bonanza la wananchi wa Tarafa ya Elerai kwenye viwanja vya Sinon Complex ukianza kwa vijana kutoka kata tano kugombea mbuzi huku Michezo ya Drafti na bao wakipata kuku zilizotolewa na Afisa Tarafa hiyo Daniel Cholobi ikiwa ni sehemu ya kuongeza ukaribu wa Serikali kwa wananchi picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Afisa Tarafa ya Elerai mwenye Fulana nyeusi akiwa kwenye uzinduzi huo kwenye viwanja vya Sinon Complex leo Jijini Arusha 

Wachezaji wa timu za kata ya Elerai wakiwa teyari kuanza mchezo wao na Kata ya Ngabobo kwenye Bonanza hilo leo viwanja vya Sinon Complex jijini Arusha.

Mchezo ukiendelea kugombea kombe la mbuzi iliyotolewa na Afisa Tarafa ya Elerai.

Sehemu ya mashabiki wakifuatilia mchezo huo wa Bonanza kwenye viwanja vya Sinon Complex leo Jijini Arusha

Mashabiki wakiwa na mgeni rasmi mwenye jezi ya klabu ya Yanga ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Jumuiya ya vijana mkoa wa Arusha wakifuatilia mchezo huo wa Bonanza la wananchi 

Mchezo wa bao ukiendelea mahindi atajishindia kuku.

Mchezo wa drafti nao haukukosekana kwenye Bonanza hilo
Mtendaji wa kata ya Ngabobo kutoka wilayani Arumeru akiteta jambo na Mjumbe wa UVCCM wakati wa Bonanza la wananchi wa Tarafa ya Elerai 


Na Ahmed Mahmoud Arusha

Wananchi wameaswa kupenda kufanya mazoezi na kushiriki katika Michezo kwa lengo la kujenga Afya zao kama Serikali inavyohimiza ikiwemo mabonanza.
Kauli hiyo Imetolewa na Afisa Tarafa la Elerai na Maratibu wa Bonanza Daniel Cholobi kwenye Bonanza alilolianda kwa lengo la kuhamasisha Michezo kwenye Tarafa hiyo na sehemu ya kukutana na wananchi kujua changamoto zao tofauti na ofisini lililofanyika kwenye uwanja wa Sinon jijini Arusha na kuzishirikisha Kata tano.
Alisema kuwa ameamua kuanzisha Bonanza hilo kuwakutanisha vijana kujenga Afya kwa wananchi wa eneo lake pia kukutana nao kwenye mazingira tofauti na Ofisi kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu na kutatua hii ikiwa ni sehemu ya ugatuzi wa madaraka kwa wananchi kuwafikia viongozi wao.
“Unajua Kuna muda wananchi wanakero na sisi tunakuwa na majukumu mengi hivyo kupitia Bonanza hili tunakutana nao kujua kero zao na kuzipatia ufumbuzi kwani wanakuwa huru na muda mzuri wa kuzizungumzia tofauti na maofisini muda unakuwa mchache kutokana na watu wengi kutaka huduma”
Kwa Upande wake Mjumbe wa uhamasishaji kutoka Jumuiya ya vijana mkoa wa Arusha alisema kuwa msingi wa jambo hilo ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kuwataka Serikali kuhakikisha inakuwa na jamii yenye Afya Bora na vijana wananshiriki Michezo kwa kuwa ni ajira na inajenga Afya.
Alisema kuwa sehemu ya michezo itasaidia vijana kuondokana na vijiwe ambavyo vinazalishwa sehemu kubwa ya matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu miongoni mwa jamii na wanaiunga mkono Serikali kuona umuhimu wa kuishirikisha kada hiyo kushiriki Michezo.