matano katika dakika 18 za kipindi cha kwanza huku Bernbard Silva
akijipatia hat-trick ya kwanza huku wenyeji hao wakiirarua Watford
katika uwanja wa Etihad.
Kikosi cha Pep Guardiola kilifunga katika
dakika ya kwanza kupitia David Silva kabla ya Sergio Aguero kuongeza
penalti naye Riyad Mahrez akifung bao la tatu.
Bernarndo Silva alifunga bao la nne kupitia kichwa huku Nicholas Otomendi akifunga bao la tano.
Baada ya kipindi cha kwanza kukamilika City iliimarisha
mashambulizi yake lakini Bernard Silva alifunga magoli mawili zaidi
huku naye Kevin de Bruyne akifunga goli la nane.
Bernardo Silva
alifunga hat-trick huku kikosi hicho cha Pep Guradiola kikijipatia
ushindi wao mkubwa zaidi tangu alipochokua hatamu 2016.
Pia
waligonga mwamba wa goli mara mbili na kuendelea kutafuta magoli mengine
hadi mwisho lakini walishindwa kuvunja rekodi ya magoli mengi zaidi
katika mechi moja.
Ushindi wa Manchester United wa magoli 9-0
dhidi ya Ipswich mwaka 1995 unasalia kuwa ushindi mkubwa zaidi katika
ligi ya Premia na City sasa inaorodheshwa kuwa timu ya saba kushinda
mechi kubwa kwa jumla ya magoli manane katika miaka ya hivi sasa.