Mechi za ligi ya mabingwa ulaya-madrid yaonja muziki wa psg, bayern yapeta

Ligi ya mabingwa Ulaya imeendelea jana kwa michezo kadhaa katika
viwanja tofauti, kundi A, Paris Saint Germain imewapiga bila huruma Real
Madrid goli 3-0, huku Galatasaray ikilazimishwa sare na Club Bruggle.

Kundi B imezikutanisha Olympiacos iliyomaliza kwa sare ya 2-2 na
Tottenham Hotspurs, huku Bayern München ikiilaza FK Crvena Zvezda goli
3-0. 

Na katika kundi C, Dinamo Zagreb imeifurumishia mvua ya magoli 4-0
Atlanta, nayo Shakhtar Donetsk imekubali kichapo cha goli 3-0 toka kwa
Manchester City. 

Michezo ya mwisho ilikuwa ni kundi D, Atletico Madrid
imetoshana nguvu ya goli 2-2 na bibi kizee wa Turin Juventus, nao
Lokomotiv Moscow ikiimaliza Bayer Leverkusen kwa goli 2-1.