Nyota wa zamani wa la lakers kobe bryant amefariki dunia katika ajali

Nyota wa mpira wa vipaku nchini Marekani Kobe Bryant amefariki dunia pamoja na wenzake wanne kwenye ajali ya helikopta iliyotokea California usiku wa leo tarehe 26 Januari 2020.

Taarifa kutoka Marekani zimeeleza kuwa Kobe Bryant alikuwa akisafiri kwa
helikopta binafsi kabla haijalipuka na kuteketea kwa moto huko
Calabasas.
Kwa mujibu wa Mamlaka jijini Los Angeles wameeleza kuwa jumla ya watu
watano walikuwa kwenye helikopta hiyo na hakuna aliyenusurika katika
ajali hiyo.
Kobe Bryant amefariki akiwa na umri wa miaka 41 akiwa na ameichezea timu
ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers nchini Marekani kwa takribani
miaka 20, hadi alipostaafu mwezi Aprili mwaka 2016


Rais
wa zamani wa Marekani Barack Obama ni  miongoni mwa watu wa awali
mashuhuri waliotuma salamu za rambirambi kufuatia kifo  hicho.