Soka: tanzania yajiweka katika mazingira magumu kufuzu fainali za (chan)

Image result for taifa stars chan
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kilichofungwa na Sudan 1 – 0 katika harakati za kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani mwakani nchini Cameroon

Tanzania imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu Fainali za Ubingwa
wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Cameroon baada ya kufungwa
1-0 nyumbani jana na Sudan katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili na
ya mwisho ya mchujo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
 Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, bao
lililoizamisha Tanzania limefungwa na Yasir Mozamil dakika ya 60
akimalizia mpira uliourudi baada ya kugonga mwamba kufuatia krosi ya
Ranadan Agab aliyefanikiwa kumtoka beki wa kulia, Boniphace Maganga. 
Sasa Tanzania wanatakiwa kwenda kushinda 2-0 ugenini kwenye mchezo wa
marudiano ambao Sudan wameomba ufanyike mjini Kampala, Uganda Oktoba 18
kwa sababu ya machafuko yanayoendelea nchini mwao.