Tigo half marathon 2020 yazinduliwa rasmi mkoani kilimanjaro

“Tunafarijika kuwa washirika #TigoKiliHalfMarathonambazo
zitawakutanisha wadau mbalimbali wakiwamo Viongozi wa Serikali na
taasisi, wanariadha wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wananchi kutoka
maeneo mbalimbali”-Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Aidan
Komba
MamaKasema: “Kuanzia sasa nazindua rasmi mbio hizi #TigoKiliHalfMarathon2020
Anna Mghwira Mkuu wa Mkoa- Kilimanjaro.  Jiandikishe Sasa! Kwani tarehe
16 Februari ndio Mwisho wa usajili. Piga *149*20# Kujiandikisha
KaribuMpakaNdani:‬ ‪“Mjisikie nyumbani mtakavyokuja katika mbio hizi na
natoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki hasa kwa
kujiandikisha mapema kushiriki mbio“ Anna Mghwira Mkuu wa Mkoa-
Kilimanjaro. ‬
Usalama Kwanza: “Naomba niwahakikishie washiriki wote usalama katika
mkoa wetu wa Kilimanjaro katika kipindi hiki cha mbio.” SSP Pili
Misungwi – Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi Moshi,Kilimanjaro.


Na TIGO, Moshi.

Mbio
maarufu za Tigo Kili Half Marathon 2020 zimezinduliwa rasmi kimkoa
katika viwanja vya Kibo Palace Homes, Mjini Moshi  kwa kushirikisha
viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro
(KAAA), waandaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali.
Akizindua
mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira aliwapongeza
wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km,
Tigo-21km Grand Malt 5km  na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi
nzuri na kusema wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu zaidi na pia
wameendelea kuutagaza Mkoa wake wa Kilimanjaro. 
Mkuu huyo wa Mkoa aliipongeza kampuni ya Tigo kwa kutoa hamasa kwa watanzania .

“Hii
iwe changamoto kuwafanya watanzania wakimbie kwakasi zaidi ili washinde
hata zawadi nyingine kubwa zinazotolewa na waandaaji.
Alitoa
wito kwa wafanya biashara kutumia fursa hii vizuri kwani wakati huu wa
Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti.
“Wenye mahoteli anzeni kufikiria kutoa ofa mbalimbali ili washiriki
watenge muda zaidi wa kukimbia lakini pia kufanya utalii na wenye mabaa
na makampuni mbalimbali mnaweza kuandaa promosheni ya wiki nzima
kutangaza biashara zenu 
Alipongeza
wadhamini wengine wakiwemo KK Security, Keys Hotel, Kilimanjaro Water,
TPC Sugar, Simba Cement, AAR, Kibo Palace, Barclays Bank na Precision
Air na waandaaji  Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive Solutions
ambao ni waratibu wa kitaifa.
  
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa  Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba
alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo
Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. Tukiongoza sokoni kwenye
mageuzi ya maisha ya kidijitali yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi
kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye
mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha – Tigo
Pesa.  
Alisema
kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi
na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka
sehemu yoyote nchini.  “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa
ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia
mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Kili Marathon Race John Addison, kuna mipango
ya kusisimua kwa ajili ya mbio hizo za mwaka huu, ikiwa ni pamoja na
wikiendi ya sherehe itakayokuwa ikifanyika mjini Moshi, bustani mwanana
ya Kilimanjaro Lager kwenye uwanja mbio zitakakomalizikia pamoja na
ubunifu mwingine kadhaa kama picha kwa ajili ya njia maalumu kwa kila
mshiriki wa marathion na half marathon.
“Washiriki waendelee kujisajili kupitia mtandao na kufanya malipo kwa kutumia credit card kupitia  www.kilimanjaromarathon.com  au
kupitia TIGO Pesa –  Pigal *149*20# kisha fuata maelekezo,” alisema na
kuongeza kwamba washiriki wajisajili mapema ili kuepuka usumbufu kwani
usajiliutafungwa Februari 7,2019 au nafasi zitakapojaa.