Mbunge wa jimbo la Wawi Pemba Ahmed Juma Ngwali Ahamia CCM

Mbunge
wa Wawi Mkoa wa Kusini Pemba (CUF), Ahmed Juma Ngwali (mwenye t-shirt
nyekundu) amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha
Mapinduzi (CCM).

Ngwali
ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 2, 2020 mbele ya Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ambaye yupo Zanzibar katika
ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya za kisiwani Pemba.

Mbunge huyo amesema anajiunga CCM kwa sababu chama hicho tawala kinapeleka maendeleo kwa wananchi.

Ngwali anaungana na wabunge wengine wanne wa CUF waliojiunga CCM ambao
ni Maulid Mtulia (Kinondoni), Ahmed Katani (Tandahimba), Abdallah Mtolea
(Temeke) na Zuberi Kuchauka (Liwale).