UTEKELEZAJI wa maamuzi yanayotolewa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) ni mdogo sana kutokana na nchi nyingi wanachama kutokuwa na utashi wa kisiasa, imeelezwa
Hukumu hizo hutolewa na Mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini hapa kutokana na malalamiko ya uvunjwaji wa haki za binadamu yaayowasilishwa na wadau mbalimbali kutoka nchi za Kiafrika.Hatua hiyo ni sawa na kuipuuza Mahakama hiyo
Kati ya nchi 30 zilizoridhia kuanzishwa kwa mahakama hiyo na nyingine nane zilizoruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO) kupeleka kesi mahakamani hapo ni Burkina Faso tu iliyotekeleza kwa asilimia 100 hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo.
“Hadi sasa ni Burkina Faso tu ndiyo iliyotekeleza kwa asilimia 100 hukumu mbili zilizotolewa na Mahakama hiyo lakini nchi nyinginezo ikiwamo Tanzania,bado,” alisisitiza Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Nouhou Diallo alipokuwa akijibu maswali kuhusu hali ya utekelezaji wa maamuzi ya mahakama hiyo mapema leo.
Katika hukumu yake, Mahakama ya Afrika ilisema kuwa, hatua ya serikali ya Kenya ya kuwafukuza watu wa jamii hiyo katika maeneo yao ya asili ya msitu wa Mau,kwa kisingizio cha kutunza misitu hiyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Jaji Kioko pia alitoa mfano wa kesi ya Tanzania kuruhusu kuwa na mgombea binafsi katika nafasi za uchaguzi ambayo ilifunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila ambako Mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za Mtikila ambaye sasa ni marehemu kuwa ni mfano wa hukumu ambazo hazijatekelezwa hadi sasa.
“Ingawa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania lilipitisha kuwa na mgombea binafsi lakini najua kuwa mchakato wa Katiba mpya Tanzania bado haujakamilika hivyo utekelezaji wa hukumu hiyo nao haujafanyika hadi sasa,” alieleza Jaji Kioko
Mapema akifungua mafunzo hayo,Rais wa Mahakama hiyo,Jaji Sylvain Ore alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wanasheria hao kutoa huduma bora kwa wateja wao ambao ni wananchi wa Afrika wanaopeleka kesi zao katika mahakama hiyo.
Nchi zilizotoa tamko hilo ni Benin,Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana,Malawi,Mali, Tunisia na Tanzania.
Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa wananchi wake kufungua kesi nyingi dhidi ya Serikali yao katika Mahakama hiyo
Kati ya kesi 178 zilizofunguliwa Mahakamani hapo tangu ilipohamia Arusha mwaka 2007, nusu ya kesi hizo zimefunguliwa na Watanzania dhidi ya Serikali yao kwa madai mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa baada ya kesi nyingi kutolewa hukumu na Mahakama za ndani.
ReplyForward
|