Misitu ya tfs yaongeza uzalishaji wa asali nchini

Na Mwandishi Wetu, Arusha
Uzalishaji wa Asali na nta  chini, umeongezeka katika
Misitu inayosimamia na Wakala wa huduma za  Misitu Tanzania(TFS) kutokana
na kuboresha uhifadhi wa mazingira na  wananchi wengi kupata elimu ya
kufuga nyuki.
Afisa Habari na uenezi wa TFS Kanda ya Magharibi, Karimu
Solyambingu akizungumza na waandishi wa habari, alisema ongezeko la uzalishaji
huo wa asali pia limechangia udhibiti wa uhabifu wa mazingira  katika
hifadhi za  misitu unaendelea kufanywa na TFS maeneo mbalimbali nchini.


Afisa Habari TFS Kanda ya Magharibi, Karimu Solyambingu

“Katika misitu ya hifadhi inayosimamiwa na TFS kanda ya
Magharibi,  katika wilaya za Sikonge, Shinyanga,  Nzega  na hata
eneo la Manyoni uzalishaji wa asali na nta umeongezeka sana”alisema
Ramadhani Mzirai Meneja wa TSF wilaya ya Shinyanga
alisema,uzalishaji wa asali katika misitu ya TFS katika wilaya hiyo,
umeongezeka kutoka  kilo 130 mwaka 2017/19 hadi kufikia kilom 700 mwaka
2018/19.
“Ongezeko hili halijawahi kutokea katika misitu yetu kwani
pia tumepata zaidi ya kilo 15 za nta na tumeweza kuwa na mizinga 140 ambayo inazalisha
lakini pia wananchi 264 kutoka vijiji 13 tuliwapa elimu na wanafuga nyuki
kisasa”alisema
Bibi nyuki wa  kituo cha TFS wilaya ya Manyoni, Jackline
Leshabari alisema alisema  uzalishaji wa asali umeongezeka wilayani
Manyoni,kutoka tani  1.7 mwaka 2017/18 hadi kufikia tangi 3.2 mwaka
2018/19.
“ongezeko hilo limetokana pia na kiasi cha mvua cha wastani
ambacho kilinyesha msimu uliopita ambacho kiliwezesha nyuki kupata maua kwa
wingi na maji kwa ajili ya kutengeneza asali “alisema
Mkuu wa TFS wilaya ya Sikonge, Haji Abdalah alisema 
kumekuwepo  na ongezeko kubwa la uzalishaji wa asali katika misitu
iliyohifadhiwa katika wilaya hiyo na mwaka 2018/19 hadi kufikia tani 100.
Afisa Nyuki wa TFS wilaya ya Shinyanga Franael Sumari 
“katika misitu hii sasa kuna zaidi ya wafugaji 1000
wanaendesha ufugaji wa kisasa lakini pia sisi kama TFS tumekuwa tukishirikiana
nao katika kuandaa mizinga na kuwapa elimu ya ufugaji nyuki “alisema
Yuda Zebedayo ambaye ni mmoja wa wafugaji wakubwa wa nyuki
wilaya ya Sokonge alisema mwaka huu anatarajia kuwa na asali  zaidi ya
120  kutokana na kuwepo msimu mzuri katika misitu ya wilaya hiyo.
Katika wilaya ya Nzega Katibu wa mbunge wa jimbo la Nzega
vijijini, Basirio Lazaro alisema uzalishaji wa wilaya hiyo, unaendelea
kuongezeka hasa baada ya TFS kuwapa  mizinga mipya 300 katika vikundi vya
ufugaji nyuki.
Mlinzi wa ofisi za TFS Nzega akionyesha baadhi ya mizinga inayoendelea kusambazwa
Lazaro alisema kila kikundi kimepewa mizinga 20 na sasa wameanza
kuvuna asali na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu, kuwa na mavuno makubwa.
“Tunapongeza TSF na Waziri wa Maliasili na Utalii, ambaye
ni mbunge wetu, Dk Hamis Kigwangalla kwa kazi nzuri ambayo wanafanya hapa nzega
kuhakikishia maisha bora wananchi kupitia asali badala ya kutegemea kilimo
pekee”alisema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala