Balozi wa tanapa atembelea hifadhi ya taifa ya mkomazi,ahimiza watanzania kutembelea hifadhi za taifa

Mkuu
wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa uzinduzi 
wa  kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
MKUU 
wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel
Mtui kushoto akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo 
katikati ni Balozi wa Tanapa Nancy Sumari na kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Same Rosemary Senyamule

Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni
ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kushoto ni Balozi
wa Tanapa Nancy Sumari na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui kushoto

Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni
ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kushoto ni Balozi
wa Tanapa Nancy Sumari na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui
Balozi
wa Tanapa nchini  Nancy Sumari katikati akiwa ameshika kikombe akiwa na
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule kulia na Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Mkomazi Abel Mtui kushoto wakati wa uzinduzi huo
Mkuu
wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule kulia akipongezana na Balozi wa
Tanapa nchini Nancy Sumari kushoto mara baada ya kufanya uzinduzi huo
kushoto ni Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui
Balozi
wa Tanapa nchini Nancy Sumari katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi Abeli Mtui kushoto wakati wa watalii wa ndani waliotembelea
hifadhi hiyo wakati wa uzinduzi huo

Muongoza
watalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kulia akitoa maelezo mafupi
kwa Balozi wa Tanapa nchini Nancy Sumary wakati aliptembelea hifadhi
hiyo

 BALOZI
wa
Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Nancy Sumari katika akiwa na baadhi ya
watalii wengine wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kutangaza
utalii wa ndani

Sehemu ya msururu wa magari ukiwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

BALOZI
wa
Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Nancy Sumari ametembelea hifadhi ya
Taifa ya Mkomazi iliyopo wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro huku
akiwahimiza watanzania kujenga mazoea ya kutembelea
hifadhi zilizopo hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio vilivyopo na
kujifunza
mambo mbalimbali ya uhifadhi wa wanyama pori.

Nancy ambaye
aliwahi kuwa Miss Tanzania 2005 na mrembo wa Dunia Afrika mwaka huo aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini iliyofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na kuzinduliwa na Mkuu
wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule.

Alisema
kwamba utalii wa ndani ni jambo muhimu sana kwa watanzania kwani unamuwezesha
kutumia muda mchache kuweza kujifunza na kujionea vivutio vilivyopo ndani ya
nchi na kuweza kuvifurahia.

“Kwa
kweli niwashukuru wananchi, Mkuu wa wilaya ya Same na Mhifadhi wa Hifadhi ya
Taifa ya Mkomazi kwa kutukaribisha mimi na familia yangu kutembelea na
kufurahia utalii wa ndani ni jambo nzuri na la kipekee sana  hivyo niendelee kuwasihi watanzania
tutembelee hifadhi zetu”Alisema

Hata
hivyo aliwakaribisha marafiki na watanzania wengine kutembelea hifadhi ya Taifa
ya Mkomazi kwani ni eneo ambalo la kipekee kutokana na kusheheni idadi kubwa ya
wanyama wakubwa na ndege ambao wageni wanakutana nao wakati tu wanapoingia
kwenye eneo la lango la geti hilo.

Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel
Mtui alisema kwamba katika kampeni hiyo wageni ambao walijiandikisha kuingia
ndani ya hifadhi ni 78 ambao kati yao kutoka wilaya ya Mwanga ni 13, Same ni 55
na Hedaru ni 10 hivyo hiyo ni idadi kubwa ya kutosha na wanategemea waliokuja
watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.

Alisema
anaimani idadi kubwa ya watalii wa ndani itazidi kuongezeka zaidi kwani wageni
waliotembelea hifadhi hiyo wataenda kuwaarifu wenzao huku wageni ambao walipata
fursa ya kutembelea hifadhi hiyo wakipiga picha na Balozi Nancy.

“Hivyo niendelee
kuwahimiza watanzania kuendelea kutembelea vivutio vya utalii ambao vipo hapa
nchini ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ambayo inavuvutio vya kipekee”Alisema

Awali
akizungumza wakati wa kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule
alkiwakaribisha Balozi huyo na familia yake na wananchi ambao tayari walianza
kujitokeza kwenye kufanya utalii wa ndani kwani wana matarajio makubwa sana na
hifadhi ya mkomazi kutokana na kuwa na vuvutio vingi vinavyopatikana na vya
kipelee ambavyo havipatikana maeneo mengine.

Mkuu huyo
wa wilaya alisema kwamba wanatagemea hifadhi ya Taifa ya mkomozi inayokuwa kwa
haraka kwa kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ikiwemo kuongeza mapato na
kukuza uchumi wa serikali na mwananchi mmoja mmoja.

“Tunaweka
nguvu nyingi kama serikali kuhakikisha mkomazi inakuwa na kupata miundombinu na
vitu vyengine vitakavyofanya watalii kuvutiw lakini pia ujio wa faru ni kuvutio
ambacho kitakuwa hakuna eneo jengine Tanzania hadi ya mkomazi kunajengwa ukuta
ambao faru watawekwa pale na upo kwenye hatua zxa mwisho za ukamilishaji”Alisema

“Kukamilika
kwake utawawezesha watanzania ambao watakuwa wakifika Mkomazi anakuwa na uhakika
wa kuona faru na itakuwa hifadhi pekee kwenye nchi ya Tanzania na nchi chache
za Afrika na wanategemea jambo hilo litasaidia kupata idadi kubwa ya wageni “Alisema
Dc huyo.

BALOZI wa Tanapa nchini Nancy Sumari kushoto akizungumza wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na kuzinduliwa na Mkuu
wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule kulia kuhusu umuhimu wa watanzania kutembelea vivutio vya utalii