Tcra watoa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum- kilimanjaro

 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akisalimiana na  Katibu wa chama cha Viziwi mkoa wa Kilimanjaro Christina Shirima .Picha zote na Vero Ignatus.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro akiendelea kusalimia na watu wenye mahitaji
maalum leo katika Semina ya Siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini (TCRA )
Baadhi
ya Watumishi wa Malaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini kutoka
katikati ni Mhandisi Mwandamizi Jan Kaaya,Wa kwanza kulia ni Lucy
Mbogoro Afisa Masoko ,pamoja na Oswarld Octavian wakiwa nje ya ukumbi wa
mkutano Mkoani Kilimanjaro ilipofanyika Semina hiyo ya siku moja ya
watu wenye mahitaji malum.
Watu
wenye  mahitaji maalumu wasioona na Viziwi wakiwa ukumbini tayari kwa
kupatiwa elimu juu ya Umuhimu wa kusajili laini za simu kwa njia ya
alama za vidole.
Mafunzo yakiendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Kilimanjaro leo.
Mkalimani
akiendelea kuwatafsiria watu wenye mahitaji maalumu wasiosikia kile
kinachoendelea katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya Kaskazini TCRA.
Watu wenye mahitaji maalumu wasisikia wakiwa makini katika mafunzo kama wanavyoonekana katika picha.
Baadhi
ya watu wenye ulemavu wa kutokuona (vipofu)wakiwa katika semina ya siku
moja iliyoandaliwa ma Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kanda ya
Kaskazini yaliyofanyika leo Mkoani Kilimanjaro.
Makundi
mawili ya watu wenye ulemavu Viziwi na Wasioona Vipofu wakiwa katika
picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira.

Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mamlaka
ya Mawasiliano nchini TCRA Kanda ya Kaskazini imefanya mkutano wa siku
moja na wadau wa mawasiliano wenye mahitaji maalum ,wakiwa katika
makundi mawili viziwi na walemavu wa kutokuona .

Akizungumza
katika mkutano huo uliofanyika Mkoani  Kilimanjaro  Mhandisi Mwandamizi
kutoka TCRA kanda ya kaskazini Jan Kaaya  amesema lengo kuu ni kutoa
elimu hususani  usajili wa kutumia alama za vidole.

Kaaya
amesekuwa  walemavu wasioona na kusikia kutokana na mahitaji waliyonayo
kwamba ni kundi ambalo linaweza kusahaulika kirahisi kutokana na hali
zao,hivyo Mamlaka hiyo ikaamua kuwapa elimu ili watambue majukumu  na
wajibu wa kusajili laini zao simu.

Akifungua
Semina hiyo siku moja Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema
matumizi ya simu yasiwe mzigo kwa wananchi haswa kwenye eneo la mihamala
ya fedha.

Tunajua
makampuni ya simu yatahitaji fedha kwaajili ya uendeshaji lakini
isiumize wananchi bali iwe gharama nafuu.” Alisema mkuu wa mkoa.

Ameyataka
makampuni yote ya simu kuangalia uwezekano wa kupeleka mawasiliano
vijijini kwani maeneo mengi wananchi wanateseka  kutoka kata kwenda
 nyingine kwenda kingine kufuata mawasiliano.

Amesisitiza
kuwa ni ukweli usiopingika kwamba asilimia kubwa ya mazao tunayotumia
mijini yanatoka kijijini,hivyo vijijini wanahitaji huduma ya mawasikiano
kwa asilimia ya juu zaidi kuliko mijini

Jana
nilikuwa kijiji cha Vudee wilaya ya Same watu wanatoka kata moja  hadi
nyingine sehemu yenye mnara ili wapate mawasiliano jambo ambalo ni
usumbufu  mkubwa kwa wananchi,nyie makampuni ya simu litazaneni jambo hili.

Kwa
upande wake Katibu wa chama cha wasiosikia mkoa wa Kilimanjaro
Christina Shirima ameishukuru TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo,pia amesema
changamoto kubea waliyonayo ni kushindwa kupata vitambulisho vya NIDA
kwa hivyo kukwamisha zoezi la kusajili laini zao za simu kwa wakati.

Nashindwa
kuelewa kwanini hivi vitambulisho vya NIDA vinachekewa kwetu sisi au
kwa vile sisi ni walemavu !aliuza mlemavu asiyesikia Ahadiel Sowene Mphuru.