Serikali yataja maeneo yanayoashiria kuvumbuliwa rasilimali ya mafuta nchini tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki
akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim
Majaliwa wakati akifungua Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania
linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)
Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.  Kongamano hilo
linawakutanisha wadau zaidi ya 592 kutoka Mataifa mbali mbali ikiwemo
Austaralia, Brazili, Canada, China, Visiwa Vya Comoro, Ghana. Mengine ni
Itali, India, Japani, Kenya, Msumbiji, Netherand, Nigeria, Afrika
Kusini, Oman, Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Nishati na Madini
Meldard Kalemani akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la
Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Serikali ya Tanzania ametaja
maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta
nchini kwa siku za usoni kupitia shughuli za utafiti zinazoendelea.
Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya
ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na Kitalu cha Eyasi Wembere
chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2.
Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora.
Dk Kalemali ametoa kauli hiyo leo
Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi.
“Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika,
Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere,
tunashukuru timu ya wataalamu ya Uganda inayosaidiana na Shirika letu
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kusaidia ushauri,”
amesema Waziri Kalemani.
Akifungua Mkutano huo Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah
Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania,
Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono
wawekezaji wanaokuja katika sekya ya Mafuta na Gesi.
“Tunawakaribisha wawekezaji zaidi
wajitokeze katika sekta hii ili kuweza kukuza uchumi wa nchi na kuzidi
kutoa ajira wa jamii,” amesema.

Meza kuu: Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim, Waziri
wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib na
Bi. Irene Batete aliyemwakilisha waziri wa Nishati Nchini Uganda. 
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama
Aboud Talib akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la
Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.

Bi. Irene Batete aliyemwakilisha Waziri wa Nishati Nchini Uganda
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi
Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere
(JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Makamu
mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania,
Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim ambao ndiyo waandaaji akizungumza wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania
linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)
Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. 
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali
mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania

Wageni na viongozi wawakilishi
Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la