Baada
ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri
wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea
wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.
Jana
jioni Alhamisi Novemba 7, 2019 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
alisema chama hicho kimejitoa na hakitashiriki uchaguzi wa serikali za
mitaa kwa kuwa ni kuhalalisha ubatili, akibainisha kuwa takribani
asilimia 85 ya wagombea wao nchi nzima wameenguliwa.

Katika
maelezo yake Jafo amesema; “Nimesikia kuwa Chama kimojawapo kimejitoa
kwenye Uchaguzi, ninachoweza kusema ni kuwa hawajawatendea haki Wananchi
wa chini kwa sababu baadhi yao walishateuliwa na wengine
wameshawasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Rufaa na tayari baadhi
ya Kamati za Rufaa zimeshaanza kutoa maamuzi juu ya rufaa hizo.

“Mtazamo
wangu maamuzi hayo yatawanyima haki na kuwadhulumu wananchi wa chini
haki yao ya kugombea na kuongoza Serikali za Mitaa ambao baadhi yao
wameshateuliwa na wengine wanasubrii rufaa zao”