Mkandarasi akabidhiwa barabara ya bypass jiji la arusha

Na Ahmed
Mahmoud Arusha
Halmashauri
ya Jiji la Arusha limepata Fedha za nyongeza kiasi cha bilion 4,106 kwa ajili
ya ujezi wa bar

Picha ya pamoja mara baada ya kukagua eneo la ujenzi wa barabara ya
Kisongo bypass itakayogharimu kiasi cha billion 4.106 hadi kukamilika
mwezi januari mwakani picha na Ahmed Mahmoud Arush
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Kulanga akimkabidhi rasmi eneo
la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass Mkandarasi wa Ujenzi
wa barabara hiyo Lang Shang ambaye ni mhandisi wa barabara wa kampuni ya
Snohydro ya China  kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara nje kidogo ya
jiji la Arusha leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Pichani ni Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay
akisikiliza taarifa kutoka kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa
pamoja na Mhandisi wa barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya
makabidhiano hayo ya ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya
jiji la Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Pichani ni Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay
akisikiliza taarifa kutoka kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa
pamoja na Mhandisi wa barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya
makabidhiano hayo ya ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya
jiji la Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha

abara ya kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa 3.44 kupitia
fedha za mradi wa TSCP inayoratibiwa na benki ya dunia chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi

Mradi huo ambao
tarehe 27 mwezi huu umekabidhiwa na Halmashauri ya  Jiji la Arusha kwa Mkandarasi  Kampuni ya Ujenzi ya Snohydro ya nchini china
utatekelezwa kwa muda wa miezi minne hadi Januari mwakani.
Akizungumza
mara baada ya kuukabidhi mradi huo kwa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha Sifael Kulanga ambaye pia ni Mwanasheria wa jiji hilo amesema kuwa mradi
huo ni wanyongeza na utatekelewa ndani ya miezi minne.
Alisema kuwa
mradi huo utasaidia kuondoa changamoto za msongamano katikati ya jiji la
Arusha na una manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na utasaidia usalama kwenye
uwanja mdogo wa ndege badala ya kukata katikati ya uwanja barabara hiyo
itasaidia kuchepuka pembezoni mwa uwanja.
“Barabara
hii ina umuhimu mkubwa sana katika uwanja wetu wa ndege na maeneo ya shule ya
sekondari na itafungua fursa kwa wanaowahi katikati ya jiji kutoka stand kubwa
ya mabasi ya mkoani inayotarajiwa kujengwa Olasit”
Kwa upande
wake Mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro watakaojenga barabara hiyo
Lang Yang Shang alisema kuwa wataifanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa na
kwa viwango vilivyowekwa na kwa ubora.
Alisema
kuwa barabara hiyo na udogo ulipo hautawapa tabu kuikamilisha ndani ya
wakati hivyo kuweza kukamilika bila kuwepo vikwazo vyovyote hivyo kuomba
ushirikiano wakati wote wa ujenzi huo.
Awali akitoa
taarifa ya mradi huo Mhandisi  Agustini
Mbuya alisema kuwa barabara hiyo ni muunganiko wa bypass na itarahisisha
mchepuko na kusaidia usalama na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa
kutenga fedha hizo.
Alisema
kuwa mradi huo utaanza ujenzi rasmi tarehe 11 mwezi ujao na leo ndio
makabidhiano kwa jiji kumkabidhi rasmi  mkarandari kwa ajili ya Ujenzi
huo wa barabara
Nae Mstahiki
meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alisema kuwa Barabara hiyo ni sehemu ya
mkataba uliosainiwa wiki iliyopita na utakuwa kielelezo cha kueleza jinsi
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa wananchi mwaka ujao jinsi serikali
ilivyotekeleza miradi.
Mwisho…..