Mwalimu wilayani maswa aishi kwenye banda la kuku.

 Na Mwandishi Wetu, Maswa

MWALIMU wa Shule ya Msingi Suligi wilayani Maswa mkoani Simiyu,Godwin Kombe amedai kuishi kwenye banda la kuku kutokana na shule hiyo kutokuwa na nyumba za kuishi walimu.

Akitoa madai yake hayo kwa Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyashimba kilichoko Kata ya Ng’hwigwa alisema kuwa amekuwa akiishi kwenye banda hilo tangu apangiwe kufundisha shule kipindi cha miezi mitano hadi sasa.

Amesema kuwa licha ya serikali kutoa fedha za Uviko 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini anashangaa kwa shule hiyo yenye upungufu wa madarasa na kutokuwa na nyumba ua Mwalimu kutopatiwa fedha.

Akizungumzia hali hiyo Mbunge,Nyongo alisema kuwa ni vizuri wananchi wakaanzisha michango kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule hiyo naye atawaunga mkono.

Pia amewataka watendaji wa Vijini na Kata kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya fedha wanazochanga kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kwani kwa kutowasomea ni kuwakatisha tamaa naatokeo yake malalamiko yanakuwa mengi