Serikali ya marekani na tanzania zazindua bweni royola *

NA MOSES MWAKIBOLWA

SERIKALI ya Marekani na Serikali ya Tanzania kwa pamoja zimezindua Bweni la Shule ya Sekondari ya Wasichana Waishio katika Mazingira Magumu Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi. Kate Somvongsiri na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe walihudhuria hafla ya kukata utepe wa bweni hilo jipya la wasichana. Ujenzi wa mabweni mapya ya Shule la Sekondari Loyola lenye thamani ya $772,000 (shiling bilioni 1.8) ulifadhiliwa na Shirika la USAID kupitia mpango wake wa Shule na Hospital za nchi za nje na utahudumia wasichana 400.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkueugenzi huyo wa USAID amesema ukosefu wa usawa wa kijinsia bado unaoendelea  nchini Tanzania na  licha ya juhudi kubwa zinazoendelea za serikali ya Tanzania na washirika wake utasaidia watoto wengi wa kike kuweza kushiriki masomo bila kikwazo chochote 

Ameongeza kuwa uandikishaji wa wavulana na wasichana kwenye shule za msingi ni karibu sawa, lakini viwango vya kumaliza sekondari kwa wasichana vinarudi nyuma

 Bi. Kate amesema ndoa za utotoni na mimba – na kutothamini mafanikio ya wasichana – ni vikwazo. Miongoni mwa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya 20-24, moja ya tano wa wasichana na theluthi moja ya wavulana humaliza sekondari.

Shule ya sekondari ya Loyola iliopo Manispaa ya Ubungo katika mtaa wa Mabibo farasi jijini Dar es Salaam inalenga kuwasaida watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao familia zao hazina uwezo wa kumudu mahitaji yao ya elimu, lakini Lengo kuu la Mpango wa USAID ASHA jijini Dar es Salaam ni kuongeza idadi ya vijana wa Kitanzania hasa wasichana waishio katika mazingira magumu kupata elimu bora

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, naibu katibu mkuu wa Wizara hiyo Prof. James Mdoe amesema ujenzi wa mabweni haya mapya utaongeza uandikishwaji na kubakia wa wasichana waishio katika mazingira magumu katika shule ya sekondari ya Loyola na kupunguza athari wanazokabiliana nazo kila siku kwenda na kurudi shuleni

Ameongeza kuwa moja ya malengo ya wizara ni kuhakikisha vijana wanapata elimu bora hutengeneza fursa za kujihusisha na kupata maarifa na ujuzi muhimu

Matokeo yake, vijana wataendeleza ustawi wa muda mrefu wa Tanzania huku wakitengeneza nchi kwa mustakabali wanaoutamani.Akizungumza katika hafla hiyo

Kwa kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa shuleni na kwenye jamii yao, wasichana wa Kitanzania wana uwezo mkubwa wa kumaliza elimu yao, kuwa na afya bora, kupata ajira, na kupunguza umaskini katika jamii