Tanzania bado inakabiliwa na majanga hatari

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Imeelezwa kuwa  bado  Tanzania inakabaliwa na changamoto mbalimbali za majanga ambayo yanaongezeka na kuathiri Jamii na kuleta maendeleo hasi.

Aidha majanga hayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuleta madhara  Kama vile upotevu na uharibifu wa miundombinu,ya umma na binafsi vifo,ukame,ulemavu wa kudumu 

Hayo yameelezwa na Meja jenerali Michael Mamunga Mkurugenzi wa idara ya menejimenti ya maafa ofisi ya waziri mkuu wakati akifungua mkutano wa wadau wa jukwaa la udhibiti wa majanga Kitaifa,Kwa niaba ya Dkt John Jingu ambaye ni Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,na uratibu

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo Serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu Katika kutekeza Sheria na sera ya maafa itaendelea na kudhibiti maafa Kwa ngazi zote pamoja na kuwa rasimu 

Alidai kuwa mpaka sasa ofisi hiyo kupitia mpango huo umeweza kuanisha majanga kumi ambayo yamekuwa yakitokea mara Kwa mara

Ametaja majanga hayo kuwa ni pamoja na  ukame,mafuriko,mioto,maporomoko,magonjwa ya mlipuko Kwa wanyama na binadamu,visumbufu vya mazao,upepo wa baharini pamoja na matetemeko

“Rasimu ya mpango mkakati imeweza kuangalia hayo yote Kwa kuwa majanga haya huja na huleta madhara makubwa sana Kwa Jamii hivyo basi ni muhimu sana Katika kushirikiana kwenye mpango

 huu”aliongeza

Aliongeza kuwa ili kukabiliana na majanga hayo ambayo yamekuwa yakitokea mara Kwa mara  mpango huo pia umeanisha majukumu 14 ambayo yanatakiwa kutekelezwa.

Alitaja majukumu ambayo sasa yanatakiwa kuchukuliwa  ambayo ni 

Huduma za afya,nishati, malazi na utunzaji wa watu,shuguli za ujenzi,usafirishaji,maelekezo ya udhibiti,uzimaji moto,uokoaji,taarifa za dharura za umma,tathimini za uharibifu

“Kila jukumu lililoanishwa hapa ipo taasisi za Serikali yenye wajibu wa Sheria na taasisi hizo zimepewa majukumu ya kutekeleza ili kupunguza majanga ya madhara endapo majanga ambayo yametokea au yatatokea Kwa kuwa lengo ni kujenga Jamii staimilivu ambayo haina majanga”aliongeza

Alihitimisha Kwa kusema kuwa ni wakati muafaka sasa wadau wa jukwaa la maafa lakini hata wale wa sekta binafsi sasa kuungana na kuwa kitu kimoja Katika kuiepusha Jamii dhidi ya majanga yatokanayo na maafa.

Naye Naibu kamisha kutoka Katika jeshi la Zima moto Charo Mangare alisema kuwa wao Kama Zima moto tayari wameshaweka mikakati mbalimbali ya kupambana na majanga ya moto 

Alitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya nyumba Kwa nyumba ili majanga yatakapotokea waweze kuchukua tahadhari 

“Ndani ya mkakati huu ambao tunauisha sasa sisi Zima moto bado tunapata majanga ya kawaida hasa kwenye mioto tunapata lakini tunawapa watanzania elimu ya kabla na baada ya janga kutokea ili linapotokea madhara yasiwe makubwa”aliongeza Mangare