Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.James Kihologwe kwa niaba ya Katibu
Mkuu Wizara hiyo Prof. Abel Makubi,akizungumza wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Upimaji na Metrolojia
kutoka TBS Mhandisi Johanes Maganga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Dodoma
sekta ya uchumi Bi Aziza Mumba,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Huduma za Ufundi wa Vifaa
Tiba-MOHCDGEC Mhandisi Valentino Mvaga mwakilishi wa Mganga Mkuu wa
Serikali,akielezea umuhimu wa wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani
yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara
(CBE) Dodoma Dkt.Kembo Bwana,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Meneja Kanda ya Kati kutoka TBS Bw.
Nickonia Mwabuka,akizungumzia umuhimu wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo
Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho
hayo wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa
yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Dkt.James Kihologwe kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof.
Abel Makub,wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika
leo Mei 20,2021 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imelitaka Shirika la Viwango nchini (TBS)
kutoa elimu kwa wananchi kuweza kutambua vipimo sahihi ni vipi na wapi
wapate hivyo vipimo sahihi.
Hayo yameelezwa leo Mei 20 2021 jijini
Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza
kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Dkt.James Kihologwe kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Abel
Makubi wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vipimo duniani.
Dkt.Kihologwe amesema TBS ina wajibu
wa kutoa elimu kwa wananchi kuweza kutambua vipimo sahihi ni vipi na
wapi wapate hivyo vipimo sahihi kwani wengi wamekuwa wakikutana na
wakati mgumu kujua vinapatikana wapi.
“Nitoe wito kwa TBS kutoa elimu kwa
wananchi kuweza kutambua vipimo sahihi ni vipi na wapi wapate hivyo
vipimo sahihi.Tunafurahi kwamba taasisi zimezungumza ninyi ni walinzi wa
Taifa mnaweka viwango vya ubora lakini pia mnasimamia hivi viwango na
si viwango tu hata wazalishaji nao pia mnawasimamia,”amesema.
Amesema Wizara ina wajibu wa kuonesha
kwamba sera, sheria ,kanuni na taratibu zinafuatwa katika masuala ya
vipimo kwa kuhakikisha mtoa huduma na elimu na ujuzi pamoja na maarifa
ya kutosha kuhusina na kupima.
“Swali lingine ambalo tunapaswa
kujiuliza ni hivi vifaa tunavyovitumia ni sahihi ni wajibu wa sisi
wenye mamalaka kusimamia pamoja na kuhakikisha wanaotoa huduma na
vifaa vyao vinaruhusu kufanya vipimo.Ni muhimu kujua nani anafanya hiyo
huduma nimefurahishwa sana na taarifa ya Mkuu a chuo kwamba wanataka
kujenga maabara ya kisasa nami nawapongeza sana.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Upimaji
na Metrolojia kutoka TBS,Mhandisi Johanes Maganga ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dkt.Athuman Ngenya amesema Shirika la Viwango
Tanzania ,licha ya kuwa dhamana kubwa ya kuthibiti ubora wa bidhaa
nchini na kutoka nje ya nchi pamoja na kumlinda mlaji pia ndio mlezi wa
viwango vya Taifa vinavyotumika katika vipimo.
“Vipimo vinaathiri afya zetu mfano
unapoenda dukani kununua panadol mbili kwa ajili ya maumivu ya kichwa
dawa hizi zinapaswa kuwa katika uzito wa miligramu 500 kwa kila kidoge.
“Viwanda vinavyozalisha vinapaswa
kuhakikisha kidonge kimoja hakizidi wala kupungua uzito ili kulinda afya
ya watumiaji na ukienda kununua na ukikuta mtengenezaji ametengeneza
chini ya hapo akakupa chini ya Milgramu 450 inamana ukikinunua
inawezekana kisiende kutibu ule ugonjwa,”amesema.
Vilevile,Mhandisi Maganga amesema
huduma bora za afya zinawezekana kwa ubora wa vipimo ambao unatolewa
hivyo kwa sasa TBS ina uwezo wa kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za
upimaji,uzito,urefu,hali joto ujazo mdogo na mkubwa,muda na masafa
mgandamizo
Naye,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Dodoma,Aziza Mumba amesema Vipimo ni muhimu na mtambuka hivyo siku hiyo
inatakiwa kutumiwa vizuri kwa wananchi kuelimishwa baadhi ya mambo
ambayo hawajui kuhusu vipimo.