Waasi wa yemen wanaoungwa mkono na iran waua wanajeshi 80

Zaidi
ya wanajeshi 80 wa Yemen wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika
shambulizi la kombora na ndege zisizokuwa na rubani linalodaiwa kufanywa
na waasi wa Houthi. 


Shambulizi
hilo linafanywa baada ya miezi kadhaa ya utulivu katikati ya vita kati
Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran na serikali ya Yemen inayotambuliwa na
jumuiya ya kimataifa inayoungwa mkono na majeshi yanayoongozwa na Saudi
Arabia. 

Vyanzo
kutoka hospitali ya Marib ambako wahanga wa shambulizi hilo
walipelekwa, vinasema wanajeshi 83 waliuawa na 148 walijeruhiwa. 

Shambulizi
hilo linakuja siku moja baada ya muungano unaosaidiwa na majeshi ya
serikali kuanzisha operesheni kubwa dhidi ya Wahouthi katika eneo la
Nihm, kaskazini mwa mji mkuu Sanaa.