Diamond platnumz apokelewa kishujaa kigoma.shuhudia hapa

Mwanamuziki
Diamond Platnumz amepokelewa na mabango wakati akiwasili stesheni ya
Nguruka Mkoani Kigoma katika kuadhimisha miaka yake kumi katika muziki.


Umati
wa watu umejitokeza katika stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma wakiwa na
mabango yaliyobeba jumbe mbalimbali kwa mwanamuziki huyo.

Moja
ya mabango hayo lilikuwa limeandikwa “Karibu Diamond kwenu Kigoma
tuijenge Kigoma, Sisi Nguruka tulishaanza ujenzi wa madarasa saba na
vyoo 12. Tunaomba tuunge mkono, watoto 494 hawana pa kusoma.”

Diamond
aliyeanza safari ya kuelekea Kigoma jana Desemba 28, 2019 akiwa na
mashabiki wake katika treni lengo lake kubwa ni kujumuika na watu wa
mkoa huo kusheherekea miaka kumi tangu kuanza muziki.

Nguruka ikiwa ndio stesheni ya kwanza unapoingia Mkoa wa Kigoma, Diamond alikutana na umati wa watu ukimsubiri.

Baada ya kuwasili eneo hilo Diamond alipanda jukwaani na kuanza kuwaimbisha wakazi hao wimbo wa Baba lao .


Hata
hivyo ilifika mahali mzuka ukampanda kweli kama moja ya kibwagizo
kilichopo katika wimbo huo kinachosema ‘mzuka ukipanda hata nguo
nitavua, nivue muone’walipoitikia mashabiki akavua fulana yake aliyokuwa
ameivaa ambapo watu wake waliichukia na baadaye kumrudishia