Chama
cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kusitisha vifurushi vya Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya Tanzania (NHIF) kwa madai kuwa vinakandamiza
wasiokuwa na uwezo.

Kauli
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho,
Dorothy Semu, alipozungumza na waandishi wa habari.

Vifurushi hivyo vilizinduliwa juzi jijini Dar es Salaam na uongozi wa
NHIF, ukieleza kuwa vimegawanywa katika makundi matatu yaliyopewa majina
ya ‘Ninajali Afya’, ‘Wekeza Afya’ na ‘Timiza Afya’.

Kwa
mujibu wa mpango huo mpya wa matibabu wa NHIF, watu wenye umri wa kati
ya miaka 18 na 35 watalipia Sh192,000 kwa mwaka kuwa katika kifurushi
cha Najali Afya Premium ama Sh384,000 cha Wekeza Afya ama Sh516,000 cha
Timiza Afya.

wenye umri mkubwa zaidi wa kuanzia miaka 36 hadi 59 watagharimia
matibabu ya mwaka mzima kwa kulipia Sh240,000 katika mpango wa Najali
Afya Premium au Sh444,000 (Wekeza Afya) au Sh612,000 (Timiza Afya).

Watu
wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea wataweza kugharimia
matibabu ya mwaka kwa kulipia kati ya Sh360,000 na Sh984,000. Bei za
vifurushi hivyo inaongezeka kulingana na idadi ya wanufaika kama mwenza
na watoto hadi wanne.

Dorothy Semu alisema kuwa kitendo cha
serikali kujiondoa kwenye kuhudumia raia wake kwenye afya kwa kutangaza
vifurushi vipya vya bima, ni kuwatenga wenye kipato cha chini.

Alisema
gharama zilizowekwa katika vifurushi hivyo vipya zinajenga matabaka
mawili katika utolewaji wa huduma za afya; la wenye nacho na wasio
nacho.

“Binadamu hachagui kuumwa au aina ya ugonjwa ambao unapaswa kuugua,
utaratibu huu wa vifurushi unachukulia kwamba suala la ugonjwa ni jambo
la hiari, kwamba mtu anaweza kuchagua kuumwa ugonjwa huu ama kuukataa
ule, hivyo atatibiwa kutokana na chaguo lake.

“Mtazamo wa namna hii ni hatari sana katika ujenzi wa jamii yenye utu,
usawa na yenye haki. Duniani kote kuna bima aina mbili, ya binafsi na ya
umma. Kiwango cha malipo ya kila mwaka kwa kila mtu ni tofauti
kulingana na vigezo tofauti.

“NHIF kimsingi ni skimu ya bima ya afya ya umma, na kwa maana hiyo
viwango vya malipo vinatokana na uwiano wa kipato cha mtu na mafao
yanapaswa kuwa sawa kwa watu wote bila kujali kiasi cha mchango
wanaotoa.

“Kitendo cha kutoa vifurushi vya malipo tofauti, na huduma kutolewa kwa
kuzingatia kifurushi, ni kitendo cha kuifanya NHIF kuwa bima binafsi na
‘kubidhaisha’ afya ya Watanzania,” alidai.

Chama hicho kilishauri kusimamishwa kwa huduma ya vifurushi hivyo vipya ili kupunguza matumizi makubwa ya rasilimali fedha.
“Kwa mfano, badala ya kuzuia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma
mbalimbali kama MRI na CT scan, serikali itoe ruzuku kwa wananchi hao
kwa kuwalipia NHIF. Huu ndiyo wajibu wa serikali kutokana na kodi
inazokusanya kutoka kwa wananchi,” alisema.

Hata
hivyo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameyajibu madai ya ACT- Wazalendo
kwa kusema kuwa Vifurushi hivi ni kupitia utaratibu wa HIYARI na sio
lazima. Pia, havijafuta Bima ya Afya ya Jamii (CHF) .

“Tusifanye siasa kwenye hili. Vifurushi
hivi ni kupitia utaratibu wa HIYARI sio lazima. Pili, havijafuta Bima ya
Afya ya Jamii (CHF) ambapo kiwango cha kuchangia kwa mwaka ni shilingi
30,000 kwa kaya ya hadi watu 6. Aidha, vifurushi vya watoto, Wakulima
nk. bado vipo.” Ameandika Ummy Mwalimu katika ukurasa wake wa Twitter wakati akipangua Hoja ya Zitto Kabwe