Afisa ustawi wa jamii kwa kushirikiana na smaujata mkoa wa shinyanga watoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya umiseta

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga Bi. Ansila Materu kwa kushirikiana na viongozi wa Kampeni ya Shujaa
wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wametoa
elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga ambao wapo
kwenye kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM.

SMAUJATA ni kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili
Nchini Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2022 chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake
na makundi maalumu ambayo inayosimamiwa na Waziri Dkt. Dorothy Gwajima.

Akitoa elimu kwa wanafunzi hao  afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu pamoja na mambo mengine amewasisitiza
kuepukana na ukatili hasa wawapo shuleni.

Amesema serikali itaendelea kuchukua
hatua kali kwa wale wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo ubakaji
na  ulawiti ambapo amewasisitiza wanafunzi
hao kuendelea kuzingatia taratibu na miongozi zilizopo shuleni ili waweze
kumaliza masomo yao salama.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi emetoa elimu ya ukatili
kwa wanafunzi hao huku akiwasisitiza kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa za
ukatili unaoendelea kufanyika katika jamii hasa wawapo shuleni ili kutokomeza
vitendo hivyo.

Madam Kisendi ametaja aina mbalimbali
za ukatili ikiwemo ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa kingono ambapo amewasihi
wanafunzi hao kuepuka ukatili na kwamba amewasisitiza kusoma kwa bidii ili waweze
kutimiza malengo yao.

“Kuna ukatili wa kimwili unafanyika huko shuleni ninyi
msikubali kufanyiwa lakini pia ukatili wa kijinsia msikubali haya yafanyike
mkiona mtoto anafanyiwa vitendo vya ukatili toa taarifa au piga simu namba ya
bure kabisa ya serikali ambayo ni 116 lakini kuna viongozi wa vijiji, mitaa
watendaji na maafisa ustawi wa jamii mtoe huko taarifa”.

“Kwa umri wetu huu mnatakiwi kusoma kwa bidii ili mtimize
ndoto zenu achana na huu ukatili wa kingono utapata ujauzito na hizi ni mimba
za utotoni ambazo zinakatisha malengo ya watu wengi kwahiyo msifanye mapenzi
mkiwa na umri mdogo someni kwanza hayo mambo kuna wakati wake”.
amesema Mwenyekiti Madam Kisendi

Aidha baadhi ya viongozi wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga akiwemo makamu mwenyekiti wa kampeni hiyo Mkoa wa Shinyanga
Mwalimu Vicent  Kanyogota nao wametoa
elimu juu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanya.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa
timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga wameshukuru na kuwapongeza viongozi wa
kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu hiyo ambapo wameahidi
kuwa mabalozi wazuri wa kupinga ukatili hasa wawapo shuleni.

Nao baadhi ya walimu na walezi wa
wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga wamepongeza kwa elimu hiyo huku
wakiwaomba viongozi wa kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na maafisa ustawi
wa jamii kuendelea kutoa elimu hiyo ya ukatili kwenye shule mbalimbali ili
kudhibiti ukatili wanaofanyiwa wanafunzi aidha bila wao kujua.

Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi akitoa elimu ya ukatili
kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo
cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi akitoa elimu ya ukatili
kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo
cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

  

Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa
timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM,
leo Jumatatu Juni 12,2023.

Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa
timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM,
leo Jumatatu Juni 12,2023.

Mwenyekiti idara ya wanawake SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga  Bi. Esther Emmanuel akitoa
elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga
waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.

Mwenyekiti idara ya wanawake SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga  Bi. Esther Emmanuel akitoa
elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga
waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.