Amani nature reserve yazindua kampeni ya ‘unlock amani

 

Mhifadhi wa Amani Nature Reserve
Bw.Bob Matunda akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Unlock
Amani inayolenga kutangaza utalii wa misitu asili na kutunza vyanzo vya
maji ili kuhakikisha misitu endelevu na upatikanaji wa maji
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo)

Mratibu wa Mradi wa Kunusuru Vyanzo
vya Maji Bonde la Wami Ruvu na Bonde la Pangani Bw.Bakari Bamba
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Unlock Amani
inayolenga kutangaza utalii wa misitu asili na kutunza vyanzo vya maji
ili kuhakikisha misitu endelevu na upatikanaji wa maji iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo)

Mtaalamu wa Miradi (UNDP) Bw.Abbas
Kitogo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Unlock Amani
inayolenga kutangaza utalii wa misitu asili na kutunza vyanzo vya maji
ili kuhakikisha misitu endelevu na upatikanaji wa maji iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mbatilo)

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Hifadhi ya misitu Asili maarufu
kama The Amani Nature Reserve imezindua kampeni ya Unlock Amani
inayolenga kutangaza utalii wa misitu asili na kutunza vyanzo vya maji
ili kuhakikisha misitu endelevu na upatikanaji wa maji.

Kampeni hiyo ni safari maalumu ya
siku tatu ambayo ni wazi kwa watu wote kwenda kuzuru Amani na kwenda
kujionea vivutio vilivyopo na pia kufahamu mikakati iliyowekwa hadi
sasa, safari hiyo imepangwa kufanyika kuanzia Agosti 27 hadi Agost 29,
2021.

Akizungumza na waandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam, Mhifadhi wa Amani Nature Reserve Bw.Bob Matunda
amesema kampeni hiyo inalenga kutumia juhudi za pamoja kuhakikisha
hifadhi hiyo inafahamika zaidi na jamii zinazoizingira kufahamu majukumu
yao katika matumizi endelevu ya ardhi.

“Tunataka kuhakikisha kuwa
tunafanya kazi kwa karibu na Serikali na wadau wengine katika kutunza
vyanzo vya mto Zigi na Ruvu na kuhakikisha Mji wa Tanga unakuwa na maji
ya kutosha muda wote”. Amesema Bw.Matunda.

Aidha ameipongeza Wizara ya Maji
kwa kupitia Mamlaka ya Pangani Water Basin, Mamlaka ya Misitu Tanzania,
Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa na Vodacom kwa kuungana katika
suala hilo la utunzaji wa vyanzo vya maji na misitu asili na tayari
mafanikio yameanza kuonekana.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa
Kunusuru Vyanzo vya Maji Bonde la Wami Ruvu na Bonde la Pangani
Bw.Bakari Bamba amesema ili kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali,
ANR ilibuni vyanzo vingine vya kipato kama vile utalii wa misitu asili,
ufugaji nyuki, samaki, vipepeo,matunda na mauana kilimo cha viungo
ikiwemo pia kutafuta masoko ya mazao yanayopatikana na upatikanaji wa
miche.

“Suala kama hili linahitaji
ushirikiano wa hali ya juu kati ya taasisi za Serikali, Sekta binafsi na
mashirika yasiyo ya Kiserikali ili kuhakikisha ardhi inatumika vizuri,
maji yanapatikana kwa uhakika na wananchi wanakuwa na maisha bora
zaidi”. Amesema Bw.Bamba.

Nae Mtaalamu wa Miradi (UNDP)
Bw.Abbas Kitogo amesema utunzaji wa vyanzo vya maji na misitu ni
miongoni mwa vipaumbele vyao na wataendelea kuunga mkono jitihada hizo.

“Tunaamini katika mazingira na
tunatoa wito kwa wadau wengine wajitokeze kujionea vivutio vilivyopo
Amani Nature Reserve “. Amesema.

Hifadhi ya misitu asilia ya Amani
imesema vyanzo vya maji na misitu asilia ni miongoni mwa vitu ambavyo
vipo hatarini kuharibiwa na zinahitajika jitihada za pamoja