Ashiriki kwenye kongamano la wanawake kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani

Na Mapuli Kitina Misalaba

Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na
ajira  Mhe. Paschal Patrobas Katambi
amewakumbusha wanawake wote hapa Nchini kuwajibikia jukumu la malezi bora na
makuzi ya watoto kama hatua ya kulinda maadili.

Katambi ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini
ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza kwenye kongamano la wanawake kuelekea kilele
cha siku ya wanawake Duniani.

Amesema ili kukabiliana na tishio la mmomonyoko wa
maadili ni wajibu wa kila mwanamke na jamii kwa ujumla kusimamia malezi na
makuzi ya watoto kwa kuzingatia maadili mema.

Katibu wa jukwaa la
uwezeshaji wanawake kiuchumi Taifa Dkt. Regina Malima amewataka wanawake
kuchukua hatua haraka katika kujikwamua kiuchumi huku akiwaomba kuendelea
kuunga mkono juhudi za serikali katika shughuli za maendeleo.

Mwenyekiti wa jukwaa la
uwezeshaji  wanawake kiuchumi Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Zezema Shilungushela
amesema jukwaa hilo limelenga kuwapataia elimu na fursa mbalimbali wanawake.

Jukwaa la wanawake Manispaa ya Shinyanga leo
limefanya kongamano kuelekea siku ya wanawake Duniani Machi 8 na kwamba kauli
mbiu ya mwaka huu inasema “Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa
na ustawi wa jamii”.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zimetolewa na
wawezeshaji ikiwemo mada ya Afya ya akili, malezi ya watoto, wanawake na
uongozi pamoja na ukatili wa kijinsia.
Awali baadhi ya viongozi wakisalimiana kabla ya kuingia ukumbini.

Buruduni ikiendelea katika kongamano la wanawake wa
jukwaa la uwezeshaji kiuchumi Manispaa ya Shinyanga, kuelekea kilele cha siku
ya wanawake Duniani.