Auawa kwa kupigwa risasi ya makalio kahama

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kijana
aliyekutwa na Kitambulisho chenye jina la Mishael Masatu (29) amefariki
dunia baada ya kupigwa risasi kwenye makalio na mlinzi wa Kampuni ya
Ulinzi Serengeti Security Services Ltd, mkazi wa mtaa wa Malunga kwenye
yard ya magari katika kisima cha mafuta cha PetroAfrica mtaa wa Mbulu
Mjini Kahama.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Oktoba 16,2019 majira ya tisa alfajiri.

“Mlinzi
wa kampuni ya Ulinzi ya Serengeti Security Services LTD  Isumail Hassan
(20) mkazi wa mtaa wa Malunga akiwa kazini hapo kisimani, alifyatua
risasi moja kutoka kwenye bunduki aina ya Shortgun yenye namba HP.9-1. 
007710112 mali ya Kampuni ya Serengeti Security Services LTD na
kumjeruhi matakoni mtu aliyekutwa na kitambulisho chenye jina la Mishael
Z. Masatu(29), mkazi wa Nyihogo mtaa wa Sazia ambaye aliingia kwenye
yard hiyo bila kibali”
,ameeleza Kamanda Abwao.

 “Chanzo
cha tukio ni majeruhi kuingia kwenye yard bila kibali na kudhaniwa kuwa
ni mwizi. majeruhi alianza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya
Halmashauri Mji wa Kahama na baadaye alifariki dunia”
,amesema Kamanda Abwao.

Amesema askari mlinzi  anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya Kahama wakati upelelezi unaendelea.