Balozi getrude mongela kuwa mgeni rasmi katika tamasha la jinsia mwaka 2019.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Jinsia TGNP Mtandao Lilian Liundi

Ikiwa imebaki siku moja kabla ya kufanyika kwa Tamasha la 14
la jinsia, TGNP Mtandao limemtaja Balozi Mama Getrude Mongela kuwa mgeni
rasmi katika tamasha la 14 linalotarajiwa kuanza September 24
hadi  27,  2019.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Lilian
Liundi wakati akizungumza na  waandishi wa habari Mapema leo Jijini Dar
es Salaam.

Akifafanua sababu za kumpa heshima Mama Mongela kuwa Mgeni Rasmi
katika Tamasha hilo la 14, Liundi amesema kuna sababu nyingi za kufanya
hivyo lakini kubwa ni harakati zake alizozifanya hadi kufikia hatua za
kuleta mageuzi ya kijinsia hapa Nchini.

“Kipekee Tanzania itakumbukwa katika historia  kwa kuweka misingi ya
usawa wa kijinsia na haki za wanawake kwani katika mkutano wa Beijing
Balozi Getrude mongela aliibuka kidedea katika mkutano huo”. alisema
Mkurugenzi

Ameongeza kuwa zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania
wanatarajiwa kushiriki Tamasha la mwaka huu, ambapo litaongozwa na kauli
mbiu inayosema ‘Wanaharakati wa Jinsia Mbioni Kubadilisha Dunia’

Lilian Liundi amesema washiriki wa tamasha hilo watakuwa ni pamoja na
wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi
mbalimbali kutoka ngazi ya halmashauri na serikali kuu, wanaharakati na
wananchi wa kawaida.

“Tunatarajia tamasha la Jinsia la Mwaka huu litakuwa la kipekee kwani
kitaifa na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya
Azimio na Mpango kazi wa Beijing amabapo vitaenda sambamba na miaka 25
ya TGNP Mtandao”.

Amesisitiza kuwa Tamasha hilo litaudhuliwa na wageni kutoka nchi kama
Rwanda, Afrika kusini, Burundi, Swizland, Kenya, Uganda, Ghana na
Zimbabwe na pia linatoa fursa kwa asasi za kiraia zilizoshiriki katika
mchakato wa Beijing kutakafari na kusherehekea uwepo wa asasi hizo kwa
zaidi ya miaka 25 ambapo azimio na mpango kazi Beijing ndiyo iliyoweka
misingii ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kidunia.

“Katika kuendelea kuenzi na kuthamini mchango wa Mama Getrude
Mongella,TGNP na Tapo la Ukombozi,tumeamua kumchagua Balozi Dr. Getrude
Mongella aliyeongoza mchakato wa Beijing na pia mchakato wa ‘Kuileta
Beijing Nyumbani’ kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Jinsia mwaka
huu”,alifafanua Liundi.

Alibainisha kuwa tamasha hilo litahusisha mawasilisho,mijadala ya
pamoja, maonesho na warsha, kusherekea mchango wa mashujaa wanawake
katika kufikia haki na usawa wa kijinsia.