Naibu
Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi
ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo
kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.

Ameyasema
hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini
kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo
ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.

“Hapa
nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote na nitamkabidhi kiongozi
wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa
sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika
wote,” amesema.

“Hizi
ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa
hatua kali na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na
mnatakiwa kuchukua hatua,” amesema Bashe.

Aidha
ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa
kwani hauwezi kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba,
ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia
wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara.