Costech yaja na ubunifu wa kifaa cha kuongeza joto kwa watoto njiti cha bei rahisi

Mkurugenzi wa Tantrade Bwana Erick Rutageruka akiwa na Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Stella Manyanya kwenye banda la Costech

Mbunifu
wa Kifaa  cha kuhifadha Joto watoto wachanga (INCUBATOR) Daktari
Emanuel Mushi Akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Stella
Manyanya namna ya kifaa kilivyo kwa ndani.
Daktari Mushi akifungua Incubator ya Joto mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda  Stella Manyanya.

 Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
kupitia Daktari Mbunifu Emanuel Mushi wamebuni mashine ya kuhifadhia
joto watoto wanaozaliwa wakiwa wamechoka na ambao hawajatimiza wakati
ili kuokoa maisha yao

Akizungumza  kwenye Viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba katika maonyesho
ya nne ya bidhaa za Viwanda vya Tanzania Mbunifu wa Kifaa hicho, Dkt.
Emanuel Mushi amesema kuwa kifaa hicho alikifanyia majaribio kwa muda
wa miaka 6 na amekipa jina la (EMBRANES WOMB) kina uwezo wa kutunza
joto la mtoto la kutosha na kinafanya kazi vizuri.
“Nilipoona tatizo la watoto njiti ni kubwa nikaona kuja na ubunifu wa
mashine hii kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto hasa upande wa
vijijini ambao wanasafirishwa kutoka hospitali ya kijiji hadi hospitali
ya mkoa ili kupata matibabu zaidi ya kiafya hivyo na joto la mtoto
linaweze kuwepo na kufanya damu itembee kwa urahisi mwilini”,amesema
Ameongeza kuwa kifaa hicho kina uwezo sawa na mashine ya kawaida ya
kuongezea joto watoto kilichopo katkika zahanati mbalimbali ambapo
ameitaka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto kumtumia
kwa ufasaha katika kuzalisha mashine nyingi zaidi na kuzisambaza katika
vituo vya afya ambayo hutoa huduma ya mama na mtoto kwa ajili ya kuokoa
maisha ya watoto wengi zaidi ili kujenga taifa lenye watoto wengi na
uchumi imara.
“Mashine hii nimeibuni mimi mwenyewe kwa taaluma yangu ya Udaktari
lengo langu ni kuokoa mamilioni ya watoto kwa kutengeneza vifaa vya
kuwaongezea joto watoto pamoja na vifaa vya kuhifadhi joto kwa ajili ya
kumsafirishia mtoto kutoka hospitali ya ya vijijini hadi hospitali ya
mkoa”,amesema 
Dkt Mushi amesema kupitia ubunifu wake huo ameweza kufanikisha
kujengwa kwa kituo cha afya cha mama na mtoto kilichopo katika mkoa wa
Manyara ambapo wanawake wengi sasa wanafika na kujifungua katika kituo
hicho.
“Kwasasa Mkoa wa Manyara umeweza kuwa na kituo cha afya cha Mama na
Mtoto na hiyo ni kutokana na kuwa na kifaa kinachoweza kuokoa maisha ya
Mtoto pia hasa aliye katika hali hatarishi hasa la kukosa joto na
kuzaliwa wakati amechoka”,ameongeza Dkt. Mushi.
Hata hivyo ameiomba serikali kuwekeza katika vifaa hivyo ili waweze
kutengeneza vifaa vingi zaidi kwajili ya kuokoa watoto wachanga
wanaokosa joto baada ya kuzaliwa.
Watoto waliozaliwa kabla ya kuhitimu muhula au wakiwa na uzani wa chini
wako katika hatari zaidi ya kufa kutokana na hipothemia, maambukizi,
matatizo ya kupumua na kutokomaa kwa viungo muhimu na Kinachofuatia ni
kuwa watoto hawa hushindwa kukabiliana na maisha nje ya uterasi na
Watoto hawa wana kiwango kidogo cha mafuta ya ngozi, hasa mafuta ya
rangi ya kahawia, mafuta haya ni muhimu sana katika kutolesha joto kwa
mtoto mzawa.