Diwani wa kata ya ndembezi mhe. victor mmanywa aanza ziara, wananchi mtaa wa butengwa walikataa jina

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Diwani wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Mhe.
Victor Thobias Mmanywa leo ameanza ziara kutembelea mitaa yote kwenye kata hiyo
kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto  mbalimbali zinazowakabili wananchi ili
kuzitafutia ufumbuzi.

Diwani huyo ametembelea mtaa wa Butengwa ambapo baadhi
ya wakazi wa mtaa huo wamempongeza kwa utendaji wake ambapo wametaja kero na
changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya miundombinu ya
barabara, maji, umeme pamoja na afya.

Wamesema mpaka sasa hakuna barabara za mitaa
zilizochongwa, wameomba kujengewa kituo cha afya karibu ili kuepusha changamoto
ya mama wajawazito kujifungulia nyumbani, wameomba kujengewa soko pamoja na
stendi katika eneo hilo huku baadhi yao wakilikata jina la Butengwa na wengine
kupendekeza jila la Mji mwema au Majiclub.

Wamesema jina la Butengwa linachangia baadhi ya
shughuli za kijamii kutofanikiwa pamoja na shughuli zingine zinazotokana na
serikali kwa Imani ya kuwa wametengwa na jamii inayowazunguka.

Wamemuomba Mh. Diwani kushughulikia changamoto
zinazowakabili ambapo  baadhi yao
wametaja changamoto za ardhi huku wakiomba wataalam kwenda kupima maeneo yao
ili wapate hati miliki.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ndembezi Mhe. Victor
Thobias Mmanywa ameahidi kutatua changamoto zilizopo kadri ya uwezo wake huku
zingine akitaja kuzifikisha sehemu husika ili ziweze kushughulikiwa kwa wakati.

Amewaomba wakazi wa mtaa wa Butengwa kuendelea
kumwamini na kushirikiana naye katika kuleta maendeleo ambapo amesema
atahakikisha changamoto zinapungua katika sekta mbalimbali ikiwemo changamoto
ya barabara, maji, afya, umeme pamoja na elimu.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal
Patrobas Katambi pamoja na viongozi wengine wa serikali katika Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga kwa kutenga na kupitisha fedha katika miradi
iliyokamilika pamoja na miradi inayoendelea ikiwemo ujenzi wa shule ya wasichana
Butengwa kata ya Ndembezi.

“Mimi
nimethamiria tena kwa thamira ya dhati kabisa kuwatumikia wananchi wa Ndembezi
katika nafasi hii na Butengwa nawaahidi sitoaangusha nitahakikisha kero
zinaenda kuisha kabla sijamaliza muda wangu Mwaka 2025, nitahakikisha
changamoto kama siyo kuisha basi tunafikia asilimia 95 lakini babari ya maji,
umeme na barabara ninaamini tutafikia asilimia 98 au kumaliza kabisa”.
amesema
Mhe, Mmanywa

“Changamoto
ya kituo cha afya tuna jengo letu wana Butengwa naomba niwahakikishie kituo
hiki tutakiendeleza kwa ajili ya kupata huduma za afya wananchi wetu wa huku
wote na bajeti ya kuanzia Mwezi wa saba mtaona, tayari kuna Milioni mia mbili
zimeshatengwa kwa ajili ya kumalizia hili jengo”

“Mmeomba
Butengwa kuwa jina hili linakasolo ndiyo maana mmetengwa nimelichukua
nitalifikisha kwenye vikao vya maamuzi, lakini pia tayari nimeomba tupewe eneo
lingine kwa ajili ya soko na changamoto ya eneo la malalo nitaendelea kuwa bega
kwa began a ninyi ili kuhakikisha hapa Butengwa mnapata eneo la malalo kwa
wenzetu wanaotangulia mbele za haki”
amesema Mhe, Mmanywa

Diwani wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Mhe.
Victor Thobias Mmanywa ameanza ziara Jumatatu Juni 5,2023 kutembelea mitaa yote
ya kata hiyo ikiwa lengo ni kupokea na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi
ambapo leo ametembelea mtaa wa Butengwa na kwamba ziara hii ni endelevu.