Dkt.bashiru amekutana na uongozi wa tgnp na kufanya mazungumzo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally
Kakurwa, leo tarehe 28 Oktoba, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na
uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mtandao wa Wanawake na
Katiba na Women Fund Tanzania (WFP).
Katika mazungumzo hayo, pamoja na
mambo mengine Mwenyekiti wa mtandao wa TGNP kwa niaba ya mashirika
mengine Bi. Asseny A. Muro amemkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake kwa
ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Katibu Mkuu akipokea mapendekezo
hayo ya Ilani, ameyasisitiza mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali
yaendelee kujikita zaidi kuhamasisha wanawake kwenye sekta za maendeleo
ili kuonesha mfano na kuaminiwa zaidi.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Lumumba Jijini Dar es salaam.