Mkurugenzi
wa Mashtaka nchini (DPP), amekata rufaa Mahakama Kuu akipinga wananchi
na waandishi wa habari kuingia kusikiliza na kuripoti kesi ya ugaidi
inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu
Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed na mwenzake 22.
amefikia uamuzi huo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde kutoa uamuzi akiruhusu waandishi
wa habari kuingia katika kesi hiyo wakati unaendelea.
iliondoa amri ya kuzuia waandishi wa habari kuandika mwenendo wa kesi
hiyo kwa sababu haijafikia katika hatua ya usikilizwaji hivyo ilisema
wanaruhusiwa kuiripoti.
rufaa iliyokatwa na DPP wanadai Mahakama ya Kisutu ilikosea kuondoa
amri ya Juni 18, mwaka 2015 ya kuzuia wananchi na waandishi kuingia
kusikiliza kesi hiyo.
washtakiwa kupitia mawakili wao, Abubakar Salim, Juma Nassoro na
wengine waliwasilisha maombi mawili mahakamani ambapo ombi la kwanza
walitaka mahakama imshauri DPP kukamilisha upelelezi ndani ya mwezi
mmoja na ombi la pili mahakama iondoe amri ya kuwazuia waandishi wa
habari kuripoti kesi hiyo.
katika uamuzi wake ilimpa njia mbili DPP, moja kukamilisha upelelezi wa
kesi hiyo ndani ya muda mfupi na njia ya pili kama anaona kuna sababu
za upelelezi kuchelewa kukamilika aliondoe shauri hilo Mahakamani,
akipata ushahidi atawashtaki tena.
wanakabiliwa na mashtaka ya kuwaingiza watu nchini kushiriki katika
vitendo vya ugaidi, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.
Mbali na Farid na Jamal Swalehe washtakiwa wengine wanaokabiliwa na
mashtaka hayo ni Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed
Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim,
Hamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othuman,
Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe.