Evariste ndayishimiye aidhinishwa kuwa mrithi wa rais pierre nkurunziza

Chama
tawala cha Burundi CNDD-FDD, kimemteua katibu wake mkuu kuwa mgombea wa
urais katika uchaguzi mkuu wa Burundi utakaofanyika Mei 2020.


Jenerali Evariste Ndayishimiye ameidhinishwa na chama kama mrithi wa Nkurunziza wa Burundi.

Meja
Jenerali Evariste Ndayishimiye ameteuliwa kama mgomba wa urais katika
uchaguzi utakaofanyika Mei 2020 kumrithi Rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza.

Jenerali
Ndayishimiye ameteuliwa Jumapili kupeperusha bendera ya chama cha
CNDD-FDD katika kikao kisicho cha kawaida kilichofanyika Gitega, mji
mkuu wa kisiasa baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa tatu ya chama
tawala cha CNDD-FDD.

Bwana Ndayishimiye ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri katika siasa za Burundi waliokaribu na Pierre Nkurunziza.

Pia
ni miongoni mwa waliokuwa waasi wa CNDD-FDD aliyejiunga baada ya
kunusurika katika mauaji ya kikabila ya wanafunzi wa Wahutu katika chuo
kikuu cha Burundi mwaka 1995.

Jenerali Ndayishimiye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD tangu Agosti 2016.

Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Waziri wa mambo ya ndani na ulinzi wa umma.

-BBC